STRAIKA wa Paris
Saint-Germain (PSG) Zlatan Ibrahimovic amethibitisha kuwa anatarajia
kuhama kikosini hapo kwenye dirisha la usajirli, msimu wa majira ya joto
(Mara tu baada ya kumaliza msimu huu).
Ibrahimovic amekuwa akiwaniwa na vilabu
vya Manchester United na Arsenal, hii itakuwa ni mafanikio ya kuimarisha
kikosi kwenye kilabu itakayofanikiwa kumsajili msimu ujao.
Straika huyo ambaye ni raia wa Sweden,
ana umri wa miaka 34 bado haijafahamika bayana kuwa nani atamsajili japo
hivi karibuni, Man United ndiyo imeonekana kupewa nafasi kubwa zaidi ya
kuidaka saini yake.
‘Sitakuwa PSG msimu ujao,’ alikaririwa na the Guardian.
Ibrahimovic amefunga magoli 377 na kufanikiwa kunyakuwa mataji makubwa 26.
‘Nimebakisha mwezi mmoja na nusu ili
kumaliza mkataba wangu. Nitafurahi nikiwa hapa. Kitakachotokea mwakani
sijui lakini nachoweza kusema sitokuwa tena hapa.’
Note: Only a member of this blog may post a comment.