Iggy Azalea Amvuruga Nick Young

Rapa, Iggy Azalea.
CALIFORNIA, Marekani
STAA wa kikapu wa timu ya L.A Leakers, Nick Young
amedaiwa kutokuwa na furaha hata ya kucheza tena mchezo huo kisa kikiwa
ni kugombana na mpenziwe, rapa, Iggy Azalea anayedai kuwa Nick
anamsaliti kimapenzi.
Staa wa kikapu wa timu ya L.A Leakers, Nick Young akiwa na mpenzi wake Iggy Azalea.
Nick ambaye ni binamu wa Mwanahip hop, Kendrick Lamar inaelezwa kuwa
kwa sasa hana amani juu ya kitu chochote ikiwemo hata kucheza kikapu na
anachokiwaza ni kumrejesha Iggy kwenye himaya yake tu.
“Anakosa sana amani anapofikiria furaha aliyokuwa nayo alipokuwa na
Iggy, anashindwa hata kufurahia anapokuwa uwanjani pale anapowaza kuwa
anaweza kumpoteza Iggy milele, kwa sasa anaona kikapu si bora sana kwake
kuliko kufikiria ni vipi anaweza kuwa na Iggy tena,” alisema rafiki wa
karibu na Nick.
USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK
TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)
Note: Only a member of this blog may post a comment.