Saturday, February 27, 2016

Anonymous

Utani Wageuka Kuwa Deal... Kampuni za Maji zajipanga Kuwekeza kwa RAY KIGOSI Baada ya Kusema Amekuwa Mweupe Kwa Sababu ya Kunywa Maji Mengi

Staa wa filamu Vicent Kigosi ‘Ray’ baada ya kudai kuwa weupe wake unatokana na kunywa maji mengi na kufanya mazoezi na siyo mkorogo, makampuni manne yanayojishughulisha na masuala ya maji yamemtaka awe balozi wao.
Ray

Akizungumza na gazeti la Mtanzania jana, Ray alisema kubadilika kwake kwa ngozi kumeleta gumzo kubwa kwake na pia kumempatia neema kutokana na makampuni hayo kutaka awe balozi wao. 
“Kunywa kwangu maji kwa wingi na kushiriki mazoezi ipasavyo ndiyo kumepekekea ngozi yangu kuwa nyororo na makampuni yaliyojitokeza kwa sasa nimewaambia wasubiri kwanza hadi nitakapokuwa tayari kuwa balozi wao,’’ alieleza Ray.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.