Saturday, December 31, 2016

Unknown

YANGA SC Hii Tema Chini Aisee!

Naona nafasi za wachezaji wengi wa Yanga wakikosa nafasi msimu unaokuja haswa kutokana na wingi wa wachezaji kila idara na kila namba katika kati ya kiwanja, hivyo jitihada zinatakiwa zifanyike kwa mchezaji mmoja mmoja kwa ajiri ya kupata namba ya kudumu.

Lwandamina ameona ni bora kuchezesha kiungo mkabaji kuliko kuchezesha kiungo mchezeshaji eneo la kukakaba kama kocha aliyepita alivyokuwa anapanga kikosi chake aliwatumia sana Kamusoko kama kiungo huku akimchezesha Mbuyu Twite kama kiungo mkabaji.

Mtiririko wa kila sehemu kujaa wachezaji kunaipa ushindani timu hiyo, wakati wa Hans Van Pluijm alimtumia sana Kamusoko akimuacha nje Niyonzima huku akimpa nafasi nyakati za mwisho katika kikosi cha kwanza lakini sasa unaweza kuona Niyonzima anapata nafasi ya kudumu huku akimuacha nje Kamusoko.

ANGALIA HAPA SASA
Niyonzima dhidi ya Kamusoko hapa kazi ipo wote wanacheza aina moja ya mpira na wote wanapiga pasi za mwisho huku Haruna Niyonzima akionekana kukubalika zaidi na mashabiki. Pembeni kuna Deus Kaseke, Juma Mahadhi pamoja na Mwashiuya angalia balaa hili lilivyo hapa kila mmoja anatafuta namba ya kudumu ya kucheza nani atolewe sadaka hakuna anayejua .


Pale kati kuna balaa lingine kuna Mkata umeme kuna Niyonzima , Kamusoko na Saidi Makapu unaonaje shughuli ya Makapu siku hizi wote hawa wanatafuta namba ya kudumu nani aanze nani asianze sio rahisi kuweza kukadiria. Nafasi ya beki kuna watu 4 Yondani, Bossou pamoja na Andrew Vicent na Nadir Haroub wote wakiwa katika wakati mzuri.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.