HABARI njema ikufikie popote ulipo ewe
shabiki wa Kanye West na tasnia nzima ya muziki wa Hip Hop. Kutokana na
kukaa kimya na kutokuachia albamu yeyote kwamiaka miwili 2014 na 2015
kitu ambacho haikuwa kawaida yake. Rapa maarufu duniani ambaye hivi
karibuni aliachia albamu yake inayoitwa ‘The Life of Pablo’, Kanye West mwishoni mwa wiki jana aliibuka na kusema anatarajia kuachia albamu tatu kwa mwaka huu kuanzia sasa.
Rapa huyo alithibitisha kauli yake hiyo alipoandika kwenye akaunti yake ya Twitter ataachia albamu tatu kwa mwaka huu wa 2016, pia aliongeza kuwa atatengeza matoleo sita ya viatu vyake vyenye lebo ya Yeezy kwa mwaka.
No more fashion calendar... I'm going Mad Max... 6 collections a year...3 albums a year
West aliachia albamu yake ya The Life of Pablo
mwezi uliopita, ambayo mapaka sasa inaendelea kufanya vizuri kwenye
vituo mbalimbali vya radio na televisheni duniani.west amesema kuwa
hakuna albamu yake hata moja kati ya hizo amabyo itakuwa kwenye mfumo wa
CD.
Miaka mitatu iliyopita kabla ya Pablo, West aliachia albamu yake ya Yeezus. Hiyo ni baada ya 2010 alipoachia My Beautiful Dark Twisted Fantasy. 2004 aliachia The College Dropout na kukaa kimya mpaka mwezi jana alipoachia The Life of Pablo.
Note: Only a member of this blog may post a comment.