T.I na Bw. Donald Trump
STORI kubwa kwa sasa nchini Marekani ni
kuhusu vuguvugu la Uchaguzi Mkuu wa nchi hiyo unaotarajiwa kufanyika
mwishoni mwa mwaka huu. Kama ilivyo Tanzania, hata nchi nyingine ni
vivyo hivyo kwani watu huonesha hisia zao kwa kuamua kusapoti mtu flani
au chama flani.
Rapa maarufu duniani T.I amekuwa ni staa
mwingine kuonesha hisia zake za kumpinga tajiri mkubwa mkubwa nchini
Bw. Donald Trump anayesaka tiketi ya kuwania urais kupitia Chama cha
Republican.
T.I. ameungana na mastaa wengine kibao
wanaompinga Trump kuwania urais wa nchi hiyo, wamo akina Chris Brown,
Mac Miller, na Frank Ocean ambao pia hivi karibuni walionekana kumpinga
Trump.
Maneno ya T.I kwenye mtandao wa Instagram:
“Sawa, Je, hivi ndivyo tunavyofanya Amerika?” “Huyu ni mwakilishi tunayemhitaji aiongoze Dunia?
Hatumhitaji mbaguzi wa rangi, dini, au
Chama iwe Democratic au Republican…… Taifa kubwa kama hili tusitegemee
haya mambo yafanyike….. Anafanya utani na demokrasia….. Haijalishi nani
utampigia kura, chama wanachokiwakilisha, au kwa nini unawachagua. Swala
ni kupiga kura!!!..

Note: Only a member of this blog may post a comment.