March 15 2016 kituo cha ITV kiliripoti taarifa kutoka visiwani Zanzibar ambapo ilidaiwa kuwa na taarifa za watu wasiojulikana kurusha bomu nyumbani kwa Kamishna wa jeshi la polisi Visiwani Zanzibar eneo la Kijichi.
Sasa taarifa niliyoipata ni kwamba
nyumba ya Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar Hamdan Omar Makame
imeripuliwa na kitu kinachosadikiwa kuwa ni bomu na watu
wasiojulikana majira ya saa 5.00 usiku huko Kijichi nje kidogo ya mji
wa Zanzibar.
Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari
Ofisini kwake Makao Makuu ya Polisi Kilimani, Kamishna Hamdani amesema
tukio hilo limeathiri sehemu ya paa la nyumba na dari na kujeruhi
baadhi ya watu waliokuwa wamelala na kusababisha hasara kubwa.
Amesema tukio hilo linafanana lile
lililotokea tarehe 03 mwezi huu katika Maskani ya CCM Kisonge Unguja
hivyo polisi inaendelea kufanya uchunguzi ikiwa ni pamoja na kuwasaka
wahalifu wanaofanya uhalifu huo.
Akizungumzia matukio mengine ya
uhalifu na kuchoma moto nyumba, maskani na kituo cha Afya huko Pemba,
alisema Jeshi la Polisi limeanza msako mkali na kuwatia mbaroni watu 31
ambao wanaendelea kuhojiwa na watakaohusika watafikishwa katika vyombo
vya sheria.
Kamishna Hamdani amewatoa hofu wananchi
kuhusu usalama wao na mali zao kuelekea uchaguzi wa marudio
utakaofanyika tarehe 20 mwezi huu na kuwepo kwa ongezeko la askari
katika maeneo mengi ya mijini na vijijini ni moja ya juhudi za
kuimarisha ulinzi na kuhakikisha uchaguzi huo utakuwa salama na
amani.
Source:Full Shangwe

Note: Only a member of this blog may post a comment.