Aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Vunjo kupitia chama cha kisiasa cha TLP Augustino Mrema, bado hajakata tamaa kuendelea na kesi yake ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa jimbo la Vunjo yaliomfanya apoteze nafasi yake ya ubunge na kuchukuliwa na James Mbatia.
“Kesi niliyofungua mahakama kuu ya Tanzania itaanza kusikilizwa March 21 2016, kesi hii wakati naifungua ilikabiliwa na upinzani mkubwa, kuna watu walitoa mapingamizi kama sita, lakini nashukuru mwenyezi mungu mapingamizi yale nimeweza kuyapangua” >>>Mrema
-via millrdayo
Note: Only a member of this blog may post a comment.