Monday, December 26, 2016

Unknown

Wafahamu Vinara wa Pasi za Mwisho Ligi Kuu ya Uingereza EPL

Ligi kuu ya England maarufu kama EPL huwa ina mabadiliko sana mchezaji anaweza akang’aa msimu mmoja msimu unaofuata akashindwa kutekeleza jukumu. Hii ndivyo ilivyo mifano mizuri Jamie Vardy, Ozil hata Hazard.

Msimu uliopita Ozil ndiye alikuwa kinara wa kutoa pasi za mwsho alipiga pasi 19 za magoli ambapo ilibaki moja afikishe rekodi ya Thiery Henry, japo haikuwa rahisi kwake kuzipata pasi zote hizo na huenda kama safu ya ushambuliaji ingetulia angeweza kuvuka rekodi ya Henry.

Hazard msimu uliopita hakuwa katika kiwango kizuri lakini msimu huu amerudi vyema sana, hivyo hivyo kwa Vardy alipata magoli 24 lakini msimu huu ametuama kama maji ya mtungi hii ndio maana halisi ya mchezo wa soka.
 EPL YA 2016-2017
Hadi sasa Kevin De Bruyne ndiye kinara wa pasi za mwisho ana nafasi za usaidizi 9 na magoli 6 ya kufunga hivyo wastani mkubwa sana kwake ikiwa bado miezi mitano ligi iishe. Huku nafasi ya pili ibashikwa na Alexis Sanchez akiwa amepata kusaidia nafasi 6 akiwa sambamba na Adam Lalana. Idadi hii kabla ya mechi za ‘Boxing Day’.

Player Country Team Assists
1. Kevin De Bruyne Belgium Manchester City 9
2. Adam Lallana England Liverpool FC 6

Nemanja Matić Serbia Chelsea FC 6

Alexis Sánchez Chile Arsenal FC 6

Wilfried Zaha Ivory Coast Crystal Palace 6
6. Coutinho Brazil Liverpool FC 5

Diego Costa Spain Chelsea FC 5

Dimitri Payet France West Ham United 5

Pedro Spain Chelsea FC 5

Matt Phillips Scotland West Bromwich Albion 5

Wayne Rooney England Manchester United 5

Gylfi Sigurðsson Iceland Swansea City 5

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.