Tuesday, March 8, 2016

Anonymous

LULU Azidi Kuchanua Nigeria... MR IBU Amtamani, Ataka Kumfuata Tanzania

Na Saleh Ally, Lagos
MWIGIZAJI maarufu wa filamu za vichekesho nchini Nigeria, John Okafor, maarufu kama Mr Ibu, amesema sasa anatamani kuja nchini Tanzania, zaidi ya hata ilivyokuwa kabla.
Akizungumza na Championi Jumatatu kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Eko jijini Lagos, Nigeria, Mr Ibu alisema awali alitamani kuja nchini Tanzania, lakini sasa ni maradufu hasa baada ya kuona msanii kinda kama Elizabeth Michael ‘Lulu’ akishinda tuzo ya Mtayarishaji Bora wa Filamu Afrika Mashariki.


“Tangu mwanzo nilikuambia nataka kuja Tanzania. Sasa hamu yangu ya kuja imezidi, nataka nitembelee Tanzania.
“Nimekuwa nikisikia sifa zake, ni nchi ambayo inaunga mkono kazi za Nollywood zikiwemo zangu. Nafikiri siku chache zijazo nitakuja,” alisema.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.