Katika hali inayoashiria kuwa CCM haijajifunza somo kuwa wananchi wamekerwa na ufisadi.
CCM
inataka kuwafanya wananchi wakose matumaini kwa serikali yao, na hivyo
kupelekea kuona kuwa juhudi za Raisi Magufuli ni hatua za kuwabana dagaa
huku wakiyaachia mapapa yakitanua mtaani.
Hatua
hiyo ya kamati kuu ni hatua ya hatari sana kwa sababu inaweka maslahi
ya watu wachache mbele kuliko Taifa, Hili ni jambo la kutisha na
kuogofya sana, kama chama kilichojinadi kurudi katika misingi
kinawalinda watu ambao Kwa kutumia nyadhifa zao wameifikisha nchi katika
hali mbaya,basi ni jambo la kuwakatisha tamaa na kuwanyong'onyesha
wananchi walioanza kurejesha imani kwa serikali yao.
DKT
Harrison Mwakyembe na Samwel Sitta ambao walikuwa mawaziri wandamizi
kwenye Serikali ya Rais Mstaafu Jakaya Kikwete ambao kwa sasa
wanatuhumiwa kwenye Kashfa za ufisadi, imefichukua kuwa uwezekano wa
kupandishwa mahakamani watu hao umeyeyuka. Mtandao umedokezwa,Anaandika
KAROLI VINSENT endelea nayo.
Sababu
iliyotajwa ya kuwaokoa mawaziri hao imetokana na Kamati kuu ya Chama
cha Mapinduzi CCM,CC kilichoketi jana kimekuja na mipango mahususi ya
kuwaokoa viongozi hao wanajiita na kuitwa ni waadilifu.
Taarifa
za kuaminika kutoka ndani ya Kikao hicho ambazo zimevuja zinasema
Kamati ya CC licha ya kujadili mambo mbali mbali ila jambo la ufisadi
ambao uliibuliwa kwenye Bandari ya Dar es Salaam pamoja na Kashfa ya
ununuzi wa mabehewa 250 ya mizigo pamoja na Mabehewa 50 ya kubebea
mafuta ambayo yamebainika kwa sasa ni mabovu nalo lilizungumziwa.
Chanzo
chetu hicho kilichokuwa ndani ya CC kimedai kuwa viongozi wa mkutano
huo walitaka suala la kuwachukulia hatua mawaziri hao waliokushika
nafasi ya wizara ya uchukuzi,litazamwe kwa umakini kwani linaweza
kukiingiza chama hicho tena kwenye mgogoro.
Yaani
CC wameona hawa wakina mwakyembe na Sitta wakipandisha Mahakamani
kujibu tuhuma hizo,basi chama chetu kitaingia kwenye mgogoro ambao
unaweza hata ukapelekea idara hata ya Ikulu ya kipindi kile kufika
mahakamani maana ufisadi huu wa Mabehewa ni mkubwa sana na umefanywa na
mtandao mkubwa ndani ya nchi kimesema Chanzo chetu hicho.
Hata
hivyo Kamati hiyo ya CC licha ya kuwakingia kifua mawaziri hao kunakuja
ni ikiwa ni siku moja kupita baada ya Rais John Magufuli kuvunja Bodi
ya Bandari ambayo Samwel Sitta wakati yupo Uchukuzi aliiunda Bodi ambayo
Magufuli ameivunja kutokana na kuhusika kwenye ufisadi,
Hatua
nyingine kwa bandari hiyo ni Rais Magufuli kutengua uteuzi wa
mkurugenzi mkuu wa Bandari Awadh Massawe baada ya kubainika pia
ameshindwa kuisimamia Bandari hiyo kwa kupelekea Ufisadi wa kutisha
ikiwemo upotevu wa Kontena zaidi ya 2000.
Sanjaria
Bandarini hapo Rais Magufuli pia alimsimamisha kazi,Katibu mkuu Wizara
ya Uchukuzi Shaaban Mwinjaka kutokana na kuitia hasara serikali ya
bilioni 16 kwenye sherika la Reli ya Kati TRL.
Taarifa
zilizopatikana wiki iliyopita zilisema Rais Magufuli alikuwa tayari
amekabidhiwa ripoti ya Ufisadi wa Bandarini na TRL ambao unatajwa kuwa
kwa namna yoyote uwezi ukawaacha mawaziri wenye dhamana ya Uchukuzi,
Hata
ufanyaje ndugu,kwenye ufisadi wa huu wa kutisha lazima Sitta na
Mwakyembe watawabwa Msalabani tu, maana wakati makontena hayo yanapoteka
kati ya 2014 na 2015 mawaziri hawa walikuwepo uchukuzi hivi hawakuyaona
haya au nao kuhusika katika kubariki wizi huu,harafu ukitoka kwenye
Bandari unakuja kwenye TRL hapa ndio kuna madudu ambayo yanawaacha
watupu,wanaojiita wapiganaji wa ufisadi amesema Mchambuzi wa Siasa
kutoka chuo kikuu cha Dodoma ,John Shilima.


Note: Only a member of this blog may post a comment.