Thursday, May 21, 2015

Anonymous

MWENYEKITI WA CHADEMA SONGEA ASIMAMISHWA KAZI KWA UFISADI WA MILIONI MOJA!

WAKATI Vyama vya siasa hapa nchini viko katika harakati ya kuwapata wagombea wa urasi, Ubunge na udiwani kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu ndani ya Chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) wilaya ya songea kunafuka moshi ambao umesababisha mwenyekiti wa Chadema wa wilaya hiyo John Mwankina kusimamishwa akituhumiwa kutumia fedha zaidi ya shilingi milioni moja bila chama hicho kujua.

Baadhi ya makada wa chama hicho wilayani Songea ambao wameomba majina yao yahifadhiwe wameiambia Nipashe kuwa ubadhilifu wa fedha hizo ulitokea mwezi mmoja uliopita ambapo Mwankina inadaiwa alichukua fedha hizo ambazo zilikuwa ni michango ya wanachama kwa ajili ya kusaidia uendeshaji ndani ya chama hicho.

Walifafanua kuwa fedha hizo baada ya kuchangwa na chama wakiwemo wadau hazikuonyeshwa wazi mpaka wananchama wenyewe walipoeleza kuwa walishachangia michango hiyo lakini hakuna taarifa ya aina yoyote iliyowekwa wazi kwa wanachama.

Walisma kuwa kufuatia kuwepo ubadhirifu huo ndani ya chama kamati ya utendaji ya Chadema wilaya ya Songea kwa hatua ya kwanza iliamua kumsimamisha uongozi mwenyekiti Mwankina wakati uchunguzi wa tuhuma hizo ukiwa unaendelea.

Kwa upande wake Katibu wa Chama cha Chadema wa wilaya ya Songea, Olais Seenga alipotakiwa kutoa ufafaunuzi wa tuhuma hizo zilizosababisha mwenyekiti wake kusimamishwa uongozi alikataa kusema lolote kwa madai kuwa jambo hilo linaendelea kufanyiwa uchunguzi.

Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na maendeleo Erneus Ngwatula alipoulizwa na Nipashe kuhusiana na kusimamishwa mwenyekiti wake wa wilaya kwa ubadhirifu alisema kuwa ofisi yake imepokea taarifa hizo Mei 1 mwaka huu na kwamba waliolalamika hawakuleta ushahidi wa aina yoyote dhidi ya tuhuma zinazomkabili Mwankina.

Amefafanua kuwa mwenyekiti Mwankina alisimamishwa na kamati ya utendaji ya wilaya ya songea kwa sababu ya matumizi mabaya ya madaraka na kwamba inadaiwa kuwa alitumia fedha za chama bila ridhaa ya wanachama ambapo mgogoro huo umetokea ofisi yake ilikuwa haifahamu lolote.

Alisema kuwa mgogoro huo wameamua kuupeleka kwenye baraza la wazee la Chadema la wilaya ya songea ambalo linapaswa kuchunguza kwa kina kwa lengo la kuumaliza mgogoro huo lakini alidai kuwa anachofahamu Mwankina anatuhumiwa kutumia fedha shilingi 265,000 na sio milioni moja kama wanavyolalamika.

Naye mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) wilaya ya Songea, Mwankina aliyesimamishwa uongozi aliiambia Nipashe kuwa hajawahi kuchukua fedha za chama kwa matumizi yake binafsi bali fedha wanazolalamikia ni shilingi 265,000 ambazo zilitumika kama posho ya kujikimu kwa baadhi ya makada wa chama hicho wilayani humo ambao walikuwa wameenda Mbeya kwenye Semina mwezi mmoja uliopita na kwamba amedai kuwa mpaka sasa yeye ndiye mwenyekiti na si vinginevyo kwani kamati ya utendaji ya chadema ya wilaya haina malamka ya kumsimamisha uongozi.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.