Inajulikana
kwamba ili chakula kikae kwa muda mrefu bila kuharibika, hasa matunda na
mboga za majani, ni lazima kihifadhiwe sehemu yenye ubaridi, kama vile
kwenye jokofu (friji). Lakini tafiti za kitaalamu zimebaini kuwa baadhi
ya vyakula havifai kuhifadhiwa kwenye friji na kwa kufanya hivyo
hupoteza ubora na kuharibika.
Katika makala haya, tunakuletea orodha ya vyakula saba ambavyo havitakiwi kuhifadhiwa kwenye jokofu:
NDIZI MBIVU: Ubora wa
tunda hili huongezeka kadiri linavyoendelea kuiva. Virutubisho
vinavyopatikana kwenye ndizi iliyoiva kidogo, iliyoiva kiasi na ile
iliyoiva sana, vinatofautiana. Ili ndizi iendelee kuiva inahitaji kukaa
kwenye joto la kawaida, unapoiweka kwenye baridi la kwenye jokofu,
haiwezi kuendelea kuiva hivyo kuwa na virutubisho hafifu.
TUFAHA: Kwa lugha
maarufu, tunda hili linajulikana kama Apple, nalo kama ilivyo kwa
nyanya, linapokaa kwa muda mrefu kwenye jokofu, hupoteza ladha na baadhi
ya virutubisho vyake. Iwapo unahitaji kula tufaha la baridi,
unaruhusiwa kuliweka kwenye jokofu kwa muda usiozidi dakika 30 tu!
VITUNGUU: Kitunguu maji
huwa hakitakiwi kuwekwa kwenye jokofu pia. Chakula au kitoweo
kilichoungwa kwa vitunguu vilivyowekwa kwenye jokofu kwa muda mrefu huwa
na ladha tofauti na pia harufu ya kitunguu kwenye chakula husikika
zaidi kuliko kawaida.
PARACHICHI: Kama ilivyo
kwa ndizi mbivu, ndivyo ilivyo kwa parachichi pia. Kulihifadhi
parachichi kwenye jokofu ni kulizuia kuendelea kuiva na hivyo kupunguza
kiwango cha virutubisho vinavyotakiwa kwenye tunda hilo.
KAHAWA: Ladha ya kahawa
huongezeka inapohifadhiwa kwenye joto la kawaida. Kahawa kabla
haijasagwa isihifadhiwe kwenye jokofu kwani ladha yake huharibika na
kuwa na ladha tofauti baada ya kuvuta na kunyonya harufu ya vyakula
vilivyomo kwenye jokofu. Unaweza kukuta kahawa ina ladha ya nyanya,
kitunguu au ndizi iwapo itahifadhiwa kwenye jokofu pamoja na vitu hivyo.
Note: Only a member of this blog may post a comment.