Pichani juu ni taswira za barabara ya Ali Hassan Mwinyi iliyopanuliwa ikiwa inatumika mbali na kujaa michanga.
BARABARA ya Ali Hassan Mwinyi kutoka Mwenge hadi Sayansi ambayo
imepanuliwa kwa maagizo ya Rais Dk. John Pombe Magufuli imefunguliwa na
inaanza kutumika na magari yote, lakini ni chafu, imejaa michanga ambayo
inahatarisha uhai wa barabara hiyo!.
Mtandao wa Global umeongea na baadhi ya watumiaji ambao wamehoji
iweje barabara hiyo iliyotengenezwa kwa mabilioni ya shilingi lakini
mamlaka husika zishindwe kusafisha tu?
Rais Dk. Magufuli aliagiza kutumika kwa shilingi bilioni nne kupanua
barabara hiyo kutoka Mwenge mataa hadi Morocco mataa na tayari kipande
cha kati ya Mwenge na Kijitonyama kimeshakamilika.
(PICHA ZOTE NA ISSA MNALLY / GPL)
(PICHA ZOTE NA ISSA MNALLY / GPL)
Note: Only a member of this blog may post a comment.