February 27 2016 Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi ilitangaza kuwasimamisha kazi watumishi wake watatu kwa tuhuma za ubadhirifu, Akizungumza na waandishi wa habari Katibu Mkuu Maimuna Tarishi amesema ‘Taasisi
ya Elimu Tanzania (TET) ilitangaza Zabuni ya kuchapa vitabu vya kiada
vya Darasa la kwanza mwaka 2015 na kampuni ya Yukos Enterprises Ltd
ikainya mshindi‘
‘Ufuatiliaji
uliofanywa na Wizara katika bohari ambayo ilikuwa ikipokea vitabu
hivyo, ulibaini kuwa vitabu vilivyowasilishwa na Kampuni hiyo kwenye
Bohari vilikuwa na kasoro‘
‘Kutokana
na mapungufu hayo, naagiza kusimamishwa kazi watumishi waliokuwa na
jukumu la kusimamia Sheria ya Maamuzi na kazi ya uchapaji wa vitabu, ili
kupisha uchunguzi zaidi ‘

Note: Only a member of this blog may post a comment.