Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania Mbwana Samatta ambaye hivi karibuni aliteuliwa na kocha wa timu ya taifa ya Tanzania kuwa nahodha mpya wa timu ya taifa ya Tanzania, yupo mji wa Genk akiendeleza maisha yake ya soka.
Samatta anacheza soka katika klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji na Jumapili ya Februry 28 saa 16:30 kwa saa za Afrika Mashariki timu yake itakuwa na mtihani mzito wa kucheza mechi dhidi ya Club Brugge ambayo inaongoza Ligi hiyo.
Mtu wangu wa nguvu kama ilikupita Samatta alifanya mahojiano na mtangazaji wa BBC Salim Kikeke
Kikeke >>>”sasa mwanangu nani anakupikia msosi” Samatta
>>> “Mimi napika mwenyewe naweza kupika wali maharage na
tambi, tambi naweza kupika kwa sababu nimekulia maisha ya kaka mashemeji
so nilikuwa naona wanavyopika hivyo tambi najua kupika vizuri”
“Huku sijawahi kuona unga wa ugali toka nimefika hivyo huwa napika wali maharage na tambi” Kikeke >>> “ungeniambia ningekuletea unga kutoka London, kuna mtu anauliza Samatta unaoa lini” Samatta >>>”hahahahah hilo swali gumu kidogo kujibuu”
Unaweza kutazama video ya dakika 2 Mbwana Samatta na Salim Kikeke walivyopiga piga stori

Note: Only a member of this blog may post a comment.