Victoria akiwa amelazwa katika hospitali ya Mwananyamala.
Stori: Imelda mtema, IJUMAA
MWANAMKE mmoja mkazi wa Kawe, jijini Dar es Salaam, aliyejulikana kwa jina la Victoria, ambaye ni bosi wa msichana wa kazi aitwaye Sewa Said amedaiwa kumfanyia unyama baada ya kummwagia maji ya moto binti huyo aliyekuwa akimdai mshahara wake wa miezi mitatu, tukio lililotokea Jumatano iliyopita.
MWANAMKE mmoja mkazi wa Kawe, jijini Dar es Salaam, aliyejulikana kwa jina la Victoria, ambaye ni bosi wa msichana wa kazi aitwaye Sewa Said amedaiwa kumfanyia unyama baada ya kummwagia maji ya moto binti huyo aliyekuwa akimdai mshahara wake wa miezi mitatu, tukio lililotokea Jumatano iliyopita.
Akizungumza na gazeti hili akiwa katika maumivu makali, Sewa ambaye
amelazwa katika Hospitali ya Mwananyamala, wodi namba 3, alisema ameishi
kwa mwanamke huyo takriban miaka minne, mwaka huu alitaka kuondoka ili
kujaribu maisha kwa namna nyingine, hivyo akadai mishahara yake ya miezi
mitatu.
“Kila nilipokuwa naulizia naambiwa nitapewa mwisho wa mwezi na wakati
huo ukifika naambiwa hadi tarehe 15, jambo hili lilikuwa linaniumiza
sana kwa sababu kila muda ukifika ananirusha,” alisema Sewa.
Msichana huyo alisema siku ya tukio alijaribu tena kuulizia kuhusu hela
zake, ambazo ni shilingi laki moja na elfu ishirini (120,000), lakini
badala ya kujibiwa mama huyo aliingia jikoni ambako alichemsha maji na
kummwagia mapajani, huku akitaka pia kumpiga na chupa ya soda.
Jeraha alilolipata baada ya kumwagiwa maji ya moto.
“Aliponimwagia maji ya moto mapajani nilikimbia nje kuomba msaada,
alinifuata akiwa na chupa ya soda na kutaka kunipiga nayo kabla ya
majirani kuingilia na kunisaidia kwa kunipaka asali na kunikimbiza kituo
cha polisi ambako nilipewa PF3 na kuletwa hapa kwa matibabu zaidi. Hadi
sasa ninasikia maumivu makali sana,” alisema.
Hadi gazeti hili linakwenda mitamboni, mwanamke huyo alikuwa bado
anasakwa na jeshi la polisi. Alipotafutwa na gazeti hili hakuweza
kupatikana.

Note: Only a member of this blog may post a comment.