Stori: Musa mateja
Ngoma ambayo Mwanamuziki Nay wa
Mitego ameiachia hivi karibuni inayokwenda kwa jina la Shika Adabu Yako,
imekaa vibaya na haiwezi kuwa poa kwa mastaa kama vile Ray, Wema na
Shetta na Basata kutokana na namna alivyowachana.
Ndani ya ngoma hiyo unasikia akimdis Ray
kuwa eti mpaka leo anaishi kwao, Shetta naye na magari ya kuazima, Wema
na mimba feki huku Basata wakipondwa kuwa wanafungia kazi za wasanii
kiholela.
Kwa floo na bit, ngoma iko poa ila kwa maneno yaliyomo ni ngumu sana traki hiyo kupigwa redioni na kufungiwa kwake kuko nje nje

Note: Only a member of this blog may post a comment.