Na Hamida Hassan
Staa wa filamu za Kibongo, Tiko
Hassan anatia huruma baada ya kuibuka na kusema kuwa unene unaomuandama
unamnyima raha kwani kila kukicha anazidi kuongezeka.
Akizungumza na Ijumaa
Tiko alisema kuwa, watu wengi wakimuona wanamshangaa mpaka anajisikia
vibaya lakini hana njia ya kufanya ili ajipunguze kwani ameshahangaika
kwenye majumba yote ya mazoezi ‘gym’ lakini hajafanikiwa.
“Mimi hapa najiona nimepungua kidogo
lakini nashangaa nikikutana na watu wananishangaa bado, najikuta nakata
tamaa, kusema ukweli hata sijui nini kitanifanya nipungue,
nachanganyikiwa mwenzenu,” alisema Tiko.

Note: Only a member of this blog may post a comment.