Staa wa Filamu Bongo, Kajala 
Masanja amesema kuwa mambo ya kimjini kama wafanyavyo mastaa wengine kwa
 sasa ameyapa mgongo kwa madai kuwa anaona anaelekea kuzeeka.
Akizungumza na mwandishi wa habari hii 
hivi karibuni, Kajala alisema kila anapojiangalia anaona kabisa 
alivyokuwa zamani sivyo alivyo sasa hivyo ana kila sababu ya kubadilika. 
“Kiukweli najiona kabisa naelekea 
kuzeeka, ule usichana unapotea hivyo ni vyema sasa mambo mengine ya 
kimjini nikayapa kisogo. Kwenda klabu usiku nimepunguza na kuna siku 
nitaacha kabisa, nguo za ajabuajabu najifikiria mara mbilimbili,” 
alisema Kajala.

Note: Only a member of this blog may post a comment.