Shilole na Nuh Mziwanda enzi wakiwa wapenzi.
Stori: Musa Mateja
Baada ya hivi
karibuni Shilole na Nuh Mziwanda kumwagana kisha kila mmoja kumwanika
mpenzi wake mpya, sasa wasanii hao imekuwa ni full kuringishiana huku
kila mmoja akidai amepata mtu sahihi
Shilole akiwa na mpenzi wake mpya.
Nuh juzikati alisema kuwa, kwa Shilole
alikuwa kapotea njia na sasa amempata mwenza sahihi aitwaye Erah Erah
huku Shilole naye akitamba kuwa, mwanaume aliyempata ambaye anafahamika
kwa jina la Medy Music ana kila sifa ya kuwa mume tofauti na Nuh.
“Hapa nimefika, huyu sasa ndiye mume wangu,” alisema Shilole kwa kifupi.
Hata hivyo, rafiki wa karibu wa Nuh
aliitonya safu hii kuwa, kila wanapokutana wasanii hao wakiwa na wapenzi
wao inakuwa ni mwendo wa kurushana roho tu.

Note: Only a member of this blog may post a comment.