TONTO DIKEH, mwigizaji maarufu wa filamu nchini
Nigeria, ambaye ni ‘mcharuko’ na ambaye alidaiwa kumchukua mume wa mtu
hivi karibuni, hivi sasa amekuwa kama mhamasishaji ambapo anatoa ujumbe
mbalimbali wa kuwatia matumaini mashabiki wake kupitia ukurasa wake wa
Instagram.
Tonto
ambaye ni mzaliwa wa Jimbo la River na aliyepata umaarufu zaidi kwa
kuigiza filamu ya ‘Dirty Secrets’, amewaasa mashabiki wake kutojali
mambo mabaya wanayosemwa na watu na kwamba “wanachokifikiria watu kuhusu
wewe si shauri lako.”
Alisisitiza kwamba, “Kuna watu fulani ambao duniani hawana la kufanya zaidi ya kutukana wenzao. Iwapo watakusema vibaya jua hawana uwezo wa kufanya mambo ya maana unayoyafanya. Watu hao watakuchekea usoni, lakini moyoni wanakuogopa.”
Ameongeza: “Watu wasioweza chochote, huyaona mabaya tu miongoni mwa mema unayofanya, wakisema wanavyoweza kuyafanya unayofanya iwapo wakitaka. Ukweli hawawezi kuyafanya hayo, kwani wangekuwa na uwezo wa kuyafanya, wangeyafanya bila ya kupiga kelele. “Wanachoweza kufanya ni kuzungumza tu. Cha kufanya ni kuzidi kung’arisha jina lako kwani watu hao ni dhahiri wanakuzimia; kwa sababu wivu na hiyana vinawamaliza.”

Note: Only a member of this blog may post a comment.