Thursday, December 3, 2015

Anonymous

Breaking News: Waziri Mkuu MAJALIWA Atinga Tena Bandarini....Angundua Upotevu wa Makontena Mengine 2431

Hii inakuwa mara ya pili kukutana na taarifa ya ziara ya ghafla iliyofanywa na Waziri Mkuu mpya wa Tanzania, Majaliwa Kassim Majaliwa… mara ya kwanza ilikuwa siku chache zilizopita ambapo aligundua upotevu wa makontena 349, watu 12 wakakamatwa na Jeshi la Polisi kwa ajili ya uchunguzi.

Kituo cha ITV kimeripoti kuwa Waziri Mkuu huyo amefanya tena ziara ya ghafla bandarini Dar pamoja na Shirika la Reli TRL na kubaini ubadhirifu mwingine, ya leo inahusu upotevu wa makontena mengine 2431 !!
Naifuatilia hii kwa ukaribu, chochote kitakachonifikia nitakufikishia wakati wowote, endelea kufuatilia hapa hapa kandiliyetu.com

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.