Stori: Dustan Shekidele, Morogoro.
AMENASWA! Hiyo ndiyo kauli unayoweza kuitumia kuelezea tukio la njemba mmoja aliyefahamika kwa jina la Mangi, mkazi wa Morogoro, anayedaiwa kuwa na kamchezo ka’ wizi, kukamatwa akiwa anaiba nguo.
Katika tukio hilo, inadaiwa Massawe alinaswa akiwa anaanua nguo zilizofuliwa na kuanikwa kwenye kamba, nyumbani kwa mwananchi mmoja aliyejitambulisha kwa jina moja la John kisha baada ya kukamatwa, alipopekuliwa kwenye kiroba alichokuwa amebeba, alikutwa akiwa na rundo la nguo nyingine alizoiba sehemu tofauti na hapo.
Taarifa zaidi zinaeleza kwamba baada ya kuwekwa chini ya ulinzi, alibebeshwa kiroba chake kilichojaa nguo zinazodaiwa kuwa ni za wizi na kuanza safari ya kumpeleka kituo cha polisi kilichokuwa umbali wa takriban kilometa mbili.
“Unajua zamani tulikuwa tunajichukulia sheria mikononi kwa sababu watu kama hawa ukiwakamata na kuwapeleka polisi, kesho unawaona wanadunda mitaani lakini sasa hivi tangu Rais (John) Magufuli aingie madarakani, tunaamini mkimpeleka mtu na uthibitisho kama huyu, lazima sheria ichukue mkondo wake,” alisema mwananchi aliyekataa kutaja jina lake.

Note: Only a member of this blog may post a comment.