Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’.
Na Musa Mateja, Risasi Jumamosi
DAR ES SALAAM: Mafahari wa Bongo Fleva,
Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ na Omar Faraj Nyembo ‘Ommy Dimpoz’
wamefika pabaya baada kutukanana mitandaoni.
Ugomvi wa wawili hao uliibuka mapema
wiki hii mara baada ya Nay kuachia wimbo wake mpya redioni uitwao Shika
Adabu Yako ambao amewachana mastaa wengi wa Bongo Muvi sambamba na Ommy
Dimpoz aliyemwambia ana shaka kuwa ana tatizo la kutokuwa na uwezo wa
kufanya tendo la ndoa.
Baada ya wimbo huo kutoka na
kumkasirisha Dimpoz ambaye aliibuka na kujibu mashambulizi mazito
mtandaoni, chanzo kimeeleza kuwa wawili hao sasa hivi wanatafutana
mtaani ili kuoneshana ubabe laivu.
“Yaani hii vita yao sasa imefika pabaya,
watakapokutana tu wawili hawa lazima pachimbike maana kila mmoja
anamuwinda mwenzake kwa wakati tofauti,” kilisema chanzo chetu.
Alipotafutwa Nay wa Mitego kuhusiana na
suala hilo alisema yeye alitegemea wimbo huo utawakera wengi lakini
ndiyo ukweli hivyo yupo tayari kwa lolote na yeye hana mpango wa kumsaka
Ommy.
“Sina habari naye huyo kama meseji imemfikia, akae kimya,” alisema Nay.
“Sina habari naye huyo kama meseji imemfikia, akae kimya,” alisema Nay.
Demu wa ommy Dimpoz

Kwa upande wake Dimpoz naye hakutaka
kukiri kuwa anamsaka Nay lakini akasema amekasirishwa sana na kitendo
cha Nay kumuimba vibaya wakati kama ni mpenzi yeye anaye na
anamridhisha.
“Yule wewe muache tu. Ameniboa sana.
Mimi kweli niwe jogoo hapandi mtungi kweli? Aache hizo, nina demu wangu
na anajua nini huwa nampatia,” alisema Dimpoz huku akimtumia mwandishi
wetu picha ya mpenzi wake pasipo kumtaja jina.

Note: Only a member of this blog may post a comment.