DAR ES SALAAM: MUIGIZAJI mkongwe wa filamu Bongo, Blandina Chagula anayefahamika kisanii kama Johari, anadaiwa kuwewesekea penzi la mbunge mmoja wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (jina linahifadhiwa) ambaye alifunga ndoa miezi michache iliyopita.
Chanzo makini kilicho karibu na msanii huyo kimeliambia gazeti hili kuwa Johari alikasirishwa na kushangazwa na hatua ya msanii mwenzake kuolewa na mbunge huyo, ilihali akijua kuwa yeye aliwahi kuishi naye kimapenzi, ingawa alikataa kuolewa naye kwa kile alichosema ‘hajatulia’.
Baada ya kunasa ushahidi unaothibitisha Johari akimzungumzia mbunge huyo kuonesha anaweweseka, gazeti hili lilimtafuta Johari na kumwuliza kuhusu tuhuma hizo, lakini msanii huyo aliruka kimanga, akidai hajawahi kuweweseka kwa penzi la mbunge huyo na wala hajawahi kuwazungumzia.

Note: Only a member of this blog may post a comment.