Stori: Boniphace Ngumije
Rapa
anayefanya poa Afrika Mashariki, Jackson Ngechu Makini ‘Prezzo’ kutoka
nchini Kenya juzi kati alitua Bongo kwa shughuli zake za kimuziki ambapo
alipata nafasi ya kukutana na mkali wa michano kutoka JPM Land, Kheli
Samil aka Mr Blue na kuingia naye Studio ya THT kuandaa ujio mpya hali
ambayo itambust mwanamuziki huyo ambaye ameonekana kupotea kimuziki.
Blue kwa sasa anafanya poa na ngoma yake
iitwayo Baki na Mimi tofauti na Prezzo ambaye ni kitambo kidogo kuwika
Kibongobongo hivyo ujio wao kwa sasa utawashitua wengi na kumuinua
upya Prezzo.
Prezzo amewahi kufanya vizuri alipokuwa
akishirikiana na msanii AY na kufanikiwa kuteka hisia za Wabongo wengi
ambapo kwa sasa amepotea.

Note: Only a member of this blog may post a comment.