Haina shaka
kwamba, Bongo Fleva sasa inakua. Inaibua vipaji vipya kila kukicha
kiasi cha kusababisha ushindani mkubwa na wakongwe ‘malejendari’.
Hii yote ni kwa sababu Bongo Fleva
imekuwa biashara kubwa inayohitaji ushindani wa hali na mali kama
ilivyokuwa kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka jana kati ya chama tawala (CCM)
na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).
Pata kujua kuwa ushindani uliopo kati ya
wakongwe na wasanii wapya Kizazi Kipya ‘KK’ ambao wanatumia muda, akili
na ubunifu kuliteka gemu. Lakini wakongwe nao wanafurukuta kuonesha
ukongwe na uwezo wao hivyo kuifanya vita hiyo kuwa tamu na iliyonoga;
AY FT DIAMOND -ZIGO REMIX
Ambwene Yessayah ni lejendari ambaye ana
singo nyingi kali kama vile Yule, Leo, Binadamu na nyinginezo. Jamaa
amelikamata gemu kwa zaidi ya miaka 15 sasa anakimbizana na vijana
wapya. Hivi karibuni ameachia remix ya ngoma yake ya Zigo akimshirikisha
Mwanamuziki wa KK, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
Navy Kenzo – Kamatia
Hili ni kundi linalounganishwa na
wapenzi ambao ni Aika Marealle na Emmanuel Mkono ‘Nahreel’ ambaye ni
muimbaji na mtayarishaji, kundi hili lipo katika upande wa KK ambapo
linazidi kufanya vizuri sana kitaifa na kimataifa katika gemu ambapo
baada ya kufanya vizuri na Wimbo wa Game kwa sasa linatesa kitaani na
wimbo mwingine wa Kamatia.
Don’t Bother -Joh Makini
John Simon naye ni mmoja wa lejendari
anayewakilisha Kundi la Weusi tangu kitambo ile akiwa River Camp
Soldiers. Aliwahi kubamba na Wimbo wa Chochote Popote kitambo kile
lakini bado anaonekana kuendelea kung’aa zaidi na hivi karibuni aliachia
Wimbo wa Don’t Bother akiwa na msanii A.K.A wa Sauz.
Utanipenda – Diamond
Staa wa Kizazi Kipya, Nasibu Abdul
‘Diamond’ anaonekana kulikamia soko zaidi ikiwemo na kupata mialiko na
tuzo mbalimbali za ndani na nje ya nchi.Kwa sasa anatesa na Wimbo wa
Utanipenda ambao unazungumzia maisha halisi kama endapo atafilisika.
Never Ever – Vee Money
Vanessa Mdee ni mwanamuziki wa kike anayefanya vizuri kwenye gemu akiwa ni KK na sasa anatamba na Wimbo wa Never Ever.
KK mwingine ni Moshi Katemi ‘Mo Music’
anayetamba na wimbo wake wa Skendo baada ya kufanya vizuri kwenye nyimbo
kama vile Basi Nenda, Mazoea na nyinginezo.
Maua Sama- Mahaba Niue
Msanii Maua Saleh Sama ni KK wa kike
anayefanya vizuri baada ya kutamba na Wimbo wa So Crazy na Let Them
Know. Kwa sasa anafanya vizuri katika Wimbo wa Mahaba Niue.
Omary Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ naye
anasimama katika kundi la KK. Alitambulika kwenye gemu akiwa na Wimbo wa
Nai Nai akiwa na Ali Kiba. Mwaka jana aliachia Wimbo wa Wanjera ambao
ulifanya vizuri sana. Kwa sasa anabamba na Wimbo wa Achia Body
unaosumbua kwenye vituo mbalimbali vya redio na runinga.
Harmonize- Aiyola
Rajabu Abdul msanii kutoka Wasafi
Classic Baby (WCB) chini ya Diamond naye anafanya vizuri sana kwa upande
wa KK kwani anaonesha wazi anataka kuwaovateki wakongwe. Anabamba
kitaani kwa sasa na Wimbo wa Aiyola.
Nako – OG
George Sixtus Mdemu ni mkongwe wa kurap
tangu enzi zile za Nako 2 Nako Soldiers mpaka Weusi ambaye kwa sasa
anakimbiza kwenye Top 10 za Kibongo na Wimbo wa Orginal ‘OG’.
MwanaFA- Asanteni kwa Kuja
Hamis Mwinjuma ni lejendari asiyechuja
tangu enzi za East Cost Team (ECT) mpaka kufanya kazi kama msanii wa
kujitegemea ‘solo artist’. Bado anaendelea kufanya vizuri kitaani na
Wimbo wa Asanteni kwa Kuja.
Jux- One More Night
Mwana KK, Juma Mussa Mpolopoto ‘Jux’
mmoja wa wakali wa RnB nchini, amewahi kutamba na nyimbo kama
Nitasubiri, Sisikii na sasa na Wimbo wa One More Night.
Jay Moe- Hili Game
Lejendari, Juma Mchopanga ‘Jay Moe’
alifanya vizuri na Wimbo wa Mvua na Jua, Kama Unataka Demu, Stori Tatu
na sasa amerejea tena na singo mpya ya Hili Gemu na imo kwenye Top 10
nchini.
Barakah Da Prince -Siwezi
Baraka Andrew ‘Barakah Da Prince’ naye
ni mmoja kati ya KK aliyeanzia kusikika kupitia Wimbo wa Siachani Naye
kisha akafanikiwa kupata Tuzo ya Kili kama Msanii Chipukizi wa mwaka
2015, kwa sasa anawatikisa malejendari na Wimbo wa Siwezi.
Chegge – Sweety Sweety
Juma Said ‘Chegge’ ni lejendari ambaye
hajawahi kuharibu kwenye nyimbo zake tangu enzi hizo akitamba na nyimbo
kama vile Lover Boy, Goodbye, Mwanayumba na nyingine nyingi. Kwa sasa
karudi na Wimbo wa Sweety Sweety kudhihirisha ukongwe wake.
Ali Kiba-Lupela
Anafahamika kama Ali Saleh Kiba ni mmoja
wa malejendari wa Muziki wa Bongo Fleva tangu enzi za Cinderella,
Sikuoni, Usiniseme, Mac Muga,Mwana na nyingine nyingi.
Kwa sasa anabamba na Wimbo wa Lupela
ambao video yake aliizindua hivi karibuni.Kikubwa na ‘malejendari’ na
Kizazi Kipya ‘KK’ ni kufanya kazi nzuri kwa lengo la kukuza na kufikisha
sanaa yetu kimataifa.

Note: Only a member of this blog may post a comment.