Wilbert Molandi na Said Ally
MSHAMBULIAJI wa Yanga, Donald Ngoma anatarajiwa kuukosa
mchezo wa kimataifa kesho Jumamosi wakati timu yake itakapopambana na
Cercle de Joachim ya Mouritius kwenye Uwanja wa Taifa katika michuano ya
Ligi ya Mabingwa Afrika.
Yanga inatarajiwa kuvaana na Cercle de Joachim baada ya awali kupata ushindi wa bao 1-0 nchini Mouritius, ambapo mfungaji alikuwa ni Ngoma.
Yanga inatarajiwa kuvaana na Cercle de Joachim baada ya awali kupata ushindi wa bao 1-0 nchini Mouritius, ambapo mfungaji alikuwa ni Ngoma.
Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro
amesema Ngoma amefiwa na mdogo wake, taarifa ambazo alizipata juzi
Jumatano mara baada ya mechi dhidi ya JKT Mlale kwenye Uwanja wa Taifa
na aliondoka alfajiri ya jana kuelekea msibani.
“Amefiwa na mdogo wake wa baba mmoja ambaye alikuwa kama mwanaye, Ngoma ndiye aliyekuwa akimlea, ameondoka leo (jana) alfajiri,” alisema Muro na kuongeza:
“Mdogo wake alifariki uwanjani wakati anatolewa kwa ajili ya kupelekwa hospitali, aligongana na mwenzake wakati wa kuwania mpira.

“Tumempatia muda wa mapumziko wa wiki moja kisha akimaliza arejee
nchini ambapo anatarajiwa kurejea kabla ya mechi dhidi ya Azam (Machi 5,
2016).”Aidha, Muro alisema kambi ya Yanga ipo kamili kwa ajili ya
mchezo huo wa kesho, ambapo pia watawakosa Haruna Niyonzima na Salum
Telela ambao ni majeruhi huku akisema kiingilio cha chini katika mchezo
wa kesho kitakuwa shilingi 5,000.Wakati huohuo, kikosi cha Cercle de Joachim kiliwasili jijini Dar es
Salaam, jana saa 12 jioni. Akizungumza na gazeti hili mara baada ya
kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, kocha wa
timu hiyo, Abdel Ben Kacem alisema:
“Tumekuja na wachezaji 21 na viongozi sita, tupo kamili na tunajua kuwa Yanga wameshinda mechi yao ya juzi. Tuna matumaini makubwa ya kupata ushindi, sisi kuwa ugenini siyo tatizo.”
“Tumekuja na wachezaji 21 na viongozi sita, tupo kamili na tunajua kuwa Yanga wameshinda mechi yao ya juzi. Tuna matumaini makubwa ya kupata ushindi, sisi kuwa ugenini siyo tatizo.”

Note: Only a member of this blog may post a comment.