Friday, February 26, 2016

Anonymous

CANNAVARO Arejea Kwa Mkwara Kilo 200

cannavaro-FILEminimizer.jpg 
Beki na nahodha wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’.

Hans Mloli, Dar es Salaam BAADA ya beki na nahodha wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ kupewa nafasi kikosini juzi Jumatano tangu arejee kufuatia kupona majeraha, ametamba kuwa yupo vizuri na atamuondoa Mtogo, Vincent Bossou na kurejea katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo.

CCC
Nadir Haroub ‘Cannavaro’.
Tangu Novemba, mwaka jana, Cannavaro alikuwa nje ya uwanja akiuguza majeraha ya kisigino kabla ya kupona hivi karibuni na kupangwa kwenye mechi hiyo ya Kombe la FA dhidi ya JKT Mlale waliyoshinda 2-1.
“Naweza kukutolea mfano wa (Vincent) Kompany yule wa Manchester City, yeye ni nahodha kama nilivyo mimi hapa na ana uwezo mzuri, inajulikana hata akikaa nje kwa majeraha lakini akirejea na kufanya mazoezi kwa bidii anarejea kwenye nafasi yake.

“Mwamuzi wa mwisho katika hili ni kocha mwenyewe lakini kwa upande wangu nipo fiti, nitaendelea kujifua na ninaamini nitarejea kwenye nafasi yangu. Uzuri ni kwamba kikosi chetu ni kipana na hata nilipoumia wengine waliziba nafasi kama kawaida, nashukuru katika hilo,” alisema Cannavaro.

Awali, Bossou alionekana hana nafasi lakini ndiye ambaye alipata nafasi ya kucheza kwa kiwango kizuri katika kipindi chote ambacho Cannavaro alikuwa nje ya uwanja hasa katika mechi ya mwisho ya ligi dhidi ya Simba waliyofanikiwa kushinda mabao 2-0.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.