Polisi wakiwa wamekaa kwenye jukwaa la juu kupinga uchaguzi kufanyika
VURUGU kubwa zimetokea wakati wa Uchaguzi wa meya wa Jiji la Dar es Salaam,mara baada ya uchaguzi huo kuhairishwa tena mwa mara ya nne leo,huku Jeshi la Polisi likivamia ukumbi wa Karimjee na kuanza kupambana na Madiwani na wabunge wa Muunganiko wa umoja wa Vyama vinavyounda UKAWA.Simulizi hii inasimuliwa na KAROLI VINSENT endelea nayo
Tukio hilo la aina yake limetokea mda huu Jijini Hapa mara baada ya mkurugenzi wa Jiji kutanga kuhairisha uchaguzi huo kwa madai ya uchaguzi huo kuwekewa pingamizi mahakamani , huku jambo hilo lilowachukiza madiwani wa UKAWA wakidai kuwa hawajapata barua hiyo ya kesi hiyo.
Wakati wakijiiandaa kufanya uchaguzi huo ukawa wenyewe ,ndipo Polisi zaidi ya 15 wakavamiaka ukumbi huo na kuwataka kuwakamata madaiwani wa ukawa ili waondoke ukumbini kuzuia uchaguzi usifanyike,jambo lilowachukiza tena ndipo Polisi wakaanza kupambana na madiwani wa Ukawa kama picha unavyoziona hapo,
Note: Only a member of this blog may post a comment.