Kwa zaidi ya miaka hamsini jimbo la Tarime mkoa wa Mara limeongozwa
na Wanaume kwa ngazi ya Ubunge , sasa time hii jimbo limeweka historia
ya kuongozwa na Mwanamke Ester Matiko.
Akiongea Exclusive Interview na ripota wa millardayo alisema..’Kwa
upande wa Tarime kwa maana ya Ubunge hakuna Mwanamke aliyewahi
kuchaguliwa kuongoza wana Tarime mimi ndio wa kwanza maana nasema
wamenipa heshima kubwa sana heshima ambayo kwakweli nitafanya kila
ninaloweza kuhakikisha kwamba natumia nafasi yangu ya Ubunge kusimamia
Serikali kuhakikisha kwamba inatimiza wajibu wa kuwatumikia watanzania‘ – Ester Matiko
Tofauti
kubwa ni kwamba nimechaguliwa na wanatarime sasa hivi nawajibika moja
kwa moja kwa wananchi wa Tarime tofauti iliyopo ni kwamba mwanzoni
nilikuwa natumikia wananchi wa mkoa wa Mara kwa maana ya majimbo 7
ambayo yamekuwa 10 sasa hivi nimekuwa mbunge wa Tarime wenye kata 8 na
maana nawajibika kuwatumikia moja kwa moja wananchi wa Tarime mjini’ – Ester Matiko
Unaweza ukabonyeza play kumsikiliza Ester Matiko

Note: Only a member of this blog may post a comment.