Saturday, December 12, 2015

Anonymous

Gardiner Afungukia Kufulia Kwa Lady Jay Dee 'JIDE'

maxresdefaultIssa Mnally Mtangazaji wa Redio EFM ya jijini Dar, Gardiner G. Habash amefungukia madai ya kwamba zilipendwa wake, Judith Wambura ‘Jide’ amefulia huku akisema anachojua ni kwamba huenda ishu ya nyota zao ndiyo chanzo.
Gardiner aliyasema hayo alipokuwa kwenye mahojiano maalum na gazeti hili ambapo alipoulizwa kama kuvunjika kwa ndoa yao ndiyo sababu ya mkewe huyo wa zamani kuyumba, alifunguka:
1901342_10152388729030025_5163726001062308245_n“Chachu ya mafanikio yake huenda ilitokana na nyota zetu kupatana na ndiyo maana mambo mengi yalienda shwari.”
Mwandishi: Una mpango gani kuhusu ndoa tena?
Gardiner: Kimya kingi kina mshindo, subirini kishindo.
Mwandishi: Unajisikiaje kuishi bila Jide?
Gardiner: Najisikia poa tu ila mwanzo nilipoachwa niliumia sana, tena sana mtu wangu.
Mwandishi: Akikuomba msamaha uko tayari kurudiana naye?
Gardiner: Unajua yule wamezaliwa mapacha, kinyota watu kama hao siyo rahisi kujishusha au kuomba msamaha hata pale inapobidi.
Mwandishi: Kuna madai kuwa baada ya ndoa yenu kwenda mrama mmeamua kugawana mali, hili lina ukweli?
Gardiner: Hilo swali naomba nisijibu tafadhali.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.