Richard Bukos na Issa Mnally
Kibano! Licha ya Rais John Pombe Magufuli kuchimba mkwara na
kutangaza kuhakikisha watoto wa Kitanzania wanapatiwa elimu ya uhakika,
tena bure kuanzia shule ya msingi hadi kidato cha nne, kijana
aliyefahamika kwa jina la Sadiq, mkazi wa Mbande-Kisiwani, Mbagala
jijini Dar anashikiliwa na polisi akituhumiwa kunaswa chumbani na denti
wa sekondari akivunja amri ya sita.
Mwanafunzi huyo akilia baada ya fumanizi.
Sadiq ambaye ni fundi wa kuchomea mageti alikamatwa juzikati akiwa
kitandani kwenye chumba chake katika nyumba moja iliyopo maeneo hayo ya
Mbande-Kisiwani akiwa na mwanafunzi huyo (jina kapuni) wa kidato cha
pili katika shule moja maarufu ya wasichana jijini Dar.
TAARIFA KUTOKA KWA MSAMARIA MWEMA
Chanzo cha tukio hilo ni taarifa ya msamaria mwema aliyepiga simu ofisi
za gazeti hili kwenye Kitengo cha Oparesheni Fichua Maovu (OFM) akieleza
jinsi ambavyo binti huyo anayetokea kusikojulikana akiwa na sare za
shule amekuwa akiingia chumbani kwa Sadiq kisha kufanya mambo yao kwa
zaidi ya saa 10 kwa siku.
Mtoa habari wetu huyo alieleza kwamba, wawili hao wakishajifungia ndani kwa muda mrefu, binti huyo huonekana akitoka kwenda bafuni kuoga huku akiwa na kanga moja.
OFM HAWALAZI DAMU
Ilielezwa kwamba, kitendo hicho kilionekana kuwakera majirani hao ambao
waliona dawa pekee ya kukomesha uovu huo ni kuwajulisha OFM ambao huwa
hawalazi damu katika eneo hilo hasa kwa kitendo hicho kinacholenga
kuwaumiza wazazi wanaosomesha mabinti zao.
Baada ya kupewa taarifa hizo, OFM ilimfungia kazi kijana huyo
anayetuhumiwa kuharibu ‘mtoto wa shule’ ambapo iliwapanga makachero
wake.
Ili kuwahi eneo la tukio, makachero hao walitumia pikipiki iendayo kwa kasi kuelekea eneo husika ambapo walifika kwenye nyumba hiyo na kujiridhisha kuwa wawili hao bado walikuwa chumbani.
Ili kuwahi eneo la tukio, makachero hao walitumia pikipiki iendayo kwa kasi kuelekea eneo husika ambapo walifika kwenye nyumba hiyo na kujiridhisha kuwa wawili hao bado walikuwa chumbani.
Nguo za mwanafunzi huyo baada ya fumanizi.
RIPOTI POLISI
Hata hivyo, kama kawaida yake, OFM ilikwenda kuripoti polisi katika Kituo cha Mbande ambapo baada ya kumweleza mkuu wa kituo hicho kisa kamili, walipewa ushirikiano mkubwa wa kumtia mbaroni mtuhumiwa huyo.

OFM ilipewa afande mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Koplo Lipingu
aliyeungana na mjumbe wa eneo hilo, Uwesu Kisoma kwa ajili ya kuongeza
nguvu kuonesha kuwa ni tukio lisilokubalika katika jamii.
BINTI KAMA ALIVYOZALIWA
Timu nzima ilipofika kwenye nyumba hiyo ilikuwa tuliii, kama vile hakuna
watu lakini mjumbe alipobisha hodi ndipo mlango ukafunguliwa na fundi
huyo aliyekuwa tayari kavaa nguo.
BINTI AANGUA KILIO
Baada ya kunaswa live na OFM kujitambulisha, binti huyo alianza kuangua
kilio kwa uchungu akiomba msamaha kwani baba yake ni mkali na anaweza
kumdhuru akisikia taarifa hizo.
HAPA KAZI TU
Kutokana na utendaji wa serikali mpya wa ‘Hapa Kazi Tu’, OFM nao
wameimarisha kikosi chao na kukataa rushwa wala aina yoyote ya kuiminya
habari hiyo na kuwaongoza afande na mjumbe kurudi kituoni kwa ajili ya
kufungua kesi.
…Akiwa na begi lake.
MAMA AANGUA KILIO
Msafara huo, ukiwa njiani, OFM walimuomba denti huyo namba za wazazi wake ambapo walimpigia baba yake lakini alisema alikuwa njiani akitokea Mtwara kisha wakampigia mama yake mlezi aliyejitambulisha kwa jina la Mwanaid ambaye baada ya kufika kituoni hapo aliangua kilio.

KESI MBAGALA-KIZUIANI
Kutokana na uzito wa kesi hiyo, Kituo Kidogo cha Polisi cha Mbande
waliihamishia katika Kituo cha Polisi cha Mbagala-Kizuiani kwa ajili ya
kufungua mashtaka.
Note: Only a member of this blog may post a comment.