Wednesday, December 9, 2015

Anonymous

Emmanuel OKWI, SIMBA SC Tena!

Emmanuel Okwi.
Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
KUNA ile methali, inasema hivi: “Banda likikushinda, jenga kibanda”. Hivi ndivyo Simba watakavyolazimika kuchagua kwa kuwa mshambuliaji wao nyota wa zamani, Emmanuel Okwi, yuko tayari kuondoka Denmark na kujiunga nao tena lakini fedha, ndiyo tatizo kubwa kwao.

Okwi amesema yuko tayari kurudi Simba, klabu ya Sonderjyske inayoshiriki Ligi Kuu Denmark ili arejee Simba, lakini yeye na klabu hiyo zimetoa masharti kwa Simba.

Sharti la kwanza ambalo wamelipata Simba kutoka kwa klabu hiyo ya Sweden ni kurudishiwa kitita cha dola 120,000 (zaidi ya Sh milioni 250) ambazo walimnunua Okwi kutoka Simba ndani ya miezi sita iliyopita.

“Tumewaambia Simba, Okwi anaweza kuja huko lakini ni lazima waturudishie fedha zetu tulizolipa kumnunua ili wamnunue kumrudisha Dar es Salaam.

“Okwi tumezungumza naye na anaonekana yuko tayari kurudi Tanzania, sisi pia hatuna tatizo,” alizungumza mmoja wa maofisa wanaoshughulikia usajili ndani ya Sonderjyske.
Sharti la pili ambalo wamepewa Simba ni kutoka kwa Okwi ambaye amesema kweli yuko tayari kurejea, lakini mshahara apewe dola 5,000 (zaidi ya Sh milioni 12).

Pia ameomba apewe fedha za ada ya usajili kama dola 30,000 (zaidi ya Sh milioni 70), jambo ambalo Simba wamelazimika kufanya mkutano wa dharura ambao ulifanyika jana jioni lengo ni kufikia uamuzi wa hilo, kwamba je, wavunje benki kumrudisha Mganda huyo matata uwanjani?

Taarifa zinaeleza, Okwi ambaye ameoa hivi karibuni, hajawa na furaha aliyoitarajia akiwa na Sonderjyske.

Lakini hata mkewe bado anaonekana kutofurahia maisha ya Denmark na akirejea Uganda, anakuwa mbali na mumewe jambo linalozidisha upweke wa Okwi ughaibuni.
Hivyo, Okwi akaona bora kurejea Afrika na timu ya kwanza kuieleza ikawa ni Simba na Sonderjyske.

Hivyo jambo hilo Simba wanatakiwa kuwa ‘sharp’ kulipatia mwafaka kabla ya Jumanne ijayo, kutokea leo ni siku sita tu zimebaki.

Championi Jumatano, limemfuta Rais wa Simba, Evans Aveva ambaye hakutaka kulifafanua kwa undani suala.“Nani kakuambia suala hilo, unajua Simba ni taasisi, hivyo ningependa kwanza mambo yashughulikiwe kabla ya kuanza kutangazwa.”

Iwapo Simba itampata Mganda huyo kwa mara nyingine, bado watakuwa na nafasi kwa kuwa imeacha wachezaji wawili, Simon Sserunkuma na Pape N’daw na imemrejesha Mkenya Paul Kiongera.

Hii itakuwa bahati kwa Simba na sasa itakuwa vigumu kwa Yanga na Azam kupata ushindi dhidi ya vijana hao wa Msimbazi kirahisi kwa kuwa anafahamika kuwa ni mshambuliaji bora sana hapa Afrika Mashariki na Kati.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.