Na Mwandishi Wetu
UPENDO! Miezi kadhaa baada ya kutofautiana juu ya ujio wa Waziri
mkuu wa zamani, Edward Lowassa katika Umoja wa Katiba ya Wananchi
(Ukawa) kati ya Mchungaji Josephat Gwajima na Dk. Wilbroad Slaa, Rais
John Pombe Magufuli amewezesha wawili hao ‘kupatana’, Risasi
Mchanganyiko linaripoti.
Kabla ya tofauti yao, Gwajima ambaye ni Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo
na Uzima na Dk. Slaa, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chadema, walikuwa ni
marafiki chanda na pete.
GWAJIMA JUMAPILI
Katika mahubiri kwa waumini wake kanisani kwake, Ubungo Maji, Dar, Jumapili iliyopita, pamoja na mambo mengine, Mchungaji Gwajima alionesha kufurahishwa kwake na utendaji kazi wa Rais Magufuli ambaye katika mwezi mmoja wa utumishi wake kama kiongozi mkuu wa nchi, amefanya maamuzi mengi magumu na yenye tija kwa jamii.
Katika mahubiri kwa waumini wake kanisani kwake, Ubungo Maji, Dar, Jumapili iliyopita, pamoja na mambo mengine, Mchungaji Gwajima alionesha kufurahishwa kwake na utendaji kazi wa Rais Magufuli ambaye katika mwezi mmoja wa utumishi wake kama kiongozi mkuu wa nchi, amefanya maamuzi mengi magumu na yenye tija kwa jamii.
Mchungaji Josephat Gwajima.
“Mheshimiwa Magufuli hayo unayoyafanya ndiyo Watanzania tumekuwa
tukiyapigia kelele miaka yote na tukaonekana wabaya. Tuko sambamba na
wewe, tunakuunga mkono, safisha nchi, usilegeze upanga wako wala usijali
vitisho vyao. Tunakuombea ushujaa zaidi na roho ya Mungu iwe nawe,”
alisema Gwajima mbele ya waumini wake.
DK. SLAA AIBUKA, AMSIFU
Muda mchache baada ya taarifa za Gwajima kuzagaa mitandaoni amemuunga
mkono Rais Magufuli, kupitia akaunti yake kwenye mtandao wa kijamii wa
Jamii Forum, Dk. Slaa aliibuka na kumfagilia kiongozi huyo wa kiroho,
kwa kitendo chake cha kuubaini ukweli.
“Sina tatizo na Gwajima wala Mtanzania yeyote kumpongeza JPM kwa
mafanikio yanayoonekana dhahiri. Akiwa kama kiongozi wa dini, alikuwa na
jukumu la kuchunga kondoo. Tulipokuwa tukipinga ufisadi tulijua nini
tunafanya, kama leo amegundua kuwa Magufuli ndiyo anafaa, ni jambo
jema,” alisema kiongozi huyo wa upinzani mwenye kuheshimika.
Dk. Wilbroad Slaa.
JUKWAA LAVAMIWA, WATAKA KUSAMEHEANA
Mara tu baada ya Dk. Slaa kuandika maneno hayo, watu mbalimbali walitoa maoni yao kutaka wawili hao kuweka kando tofauti zao, badala yake wote waungane na kumpa moyo wa kufanya kazi, Rais Magufuli.
Mara tu baada ya Dk. Slaa kuandika maneno hayo, watu mbalimbali walitoa maoni yao kutaka wawili hao kuweka kando tofauti zao, badala yake wote waungane na kumpa moyo wa kufanya kazi, Rais Magufuli.
“Mimi nadhani huu siyo wakati wa kuendeleza malumbano, wakati ule
hawa watu walitofautiana kwa vile kila mmoja alikuwa analipigania taifa.
Sasa kama leo wamekutana na wote wanakubaliana na kazi ya Magufuli, ni
jambo jema sana. Wasahau yaliyopita, tugange yajayo,” aliandika mtu
mmoja anayejiita ChaArusha.
RISASI LAZAMA MTAANI
Baada ya jitihada kubwa kufanyika ili kuwapata viongozi hao wawili
kuzungumzia suala hilo, gazeti hili liliamua kuingia mtaani ili kupata
maoni ya wananchi juu ya wawili hao wawili, kila mmoja kwa wakati wake
kuonekana kukunwa na kazi ya Rais Magufuli.
Japhet Kimaro, aliyejitambulisha kama mfuasi wa Chadema, alisema kama
mtu analipenda taifa hili, hawezi kubeza kazi inayofanywa na Rais
Magufuli kwa sasa.
“Sikia, mimi nilimwelewa sana Gwajima wakati ule, kwa sababu sijui
ungeniambia nini kuhusu Lowassa, lakini baada ya huu mwezi mmoja, hakika
nimemkubali Magufuli, Mungu amlinde na simlaumu Gwajima kwa sababu hata
mimi nilikuwa kama yeye, sisi hatuichukii CCM, bali tunachukia watu
wanaokitumia chama hicho kuiba, kujineemesha.
“Ninajua Dk. Slaa ana uchungu na nchi hii, Gwajima naye anakerwa na
maovu ya watu wa serikali, tunachotaka rasilimali zetu zitufaidishe
wote, kama anavyotaka rais Magufuli, nawasihi viongozi wangu hawa
wamalize tofauti zao, tupige kazi,” alisema msomaji mmoja.
Naye Monalisa Blaise aliyejitambulisha kama Ukawa Kindakindaki,
alisema hana tatizo na Magufuli, kwani siku zote wapinzani walitaka
mchapakazi wa kuwaondoa mafisadi katika rasilimali za nchi.
“Tokea mwanzo tulijua Magufuli ni mchapakazi, kama alivyokuwa mgombea
wetu, lakini tulimtaka zaidi Lowassa kwa sababu ametoka nje ya mfumo,
tuliamini mgombea wa CCM ataendeleza ulaji, lakini sasa ni tofauti
kabisa, nadhani watu wote wanaoitakia mema nchi yetu ni lazima tuwe
pamoja na rais kwa kauli mbiu yake ya hapa kazi tu.”
GWAJIMA, DK. SLAA WAMFUATA PROFESA LIPUMBA
Kitendo cha viongozi hao wawili kusifia utendaji kazi wa kasi wa Rais
John Magufuli, ni kama kufuata nyayo za aliyekuwa mwenyekiti wa zamani
wa Cuf, Profesa Ibrahim Lipumba ambaye siku chache zilizopita, alikwenda
Ikulu jijini Dar kumpongeza kwa mwanzo mzuri wa utawala wake.
Profesa Lipumba ambaye alijiuzulu cheo chake hicho kabla ya uchaguzi
mkuu, alikuwa mpinzani wa kwanza kuelezea waziwazi kufurahishwa na
utendaji kazi wa Rais Magufuli ambaye amekuwa akisifiwa kila kukicha
kutokana na kasi yake inayowavutia wengi.

Note: Only a member of this blog may post a comment.