Na Brighton Masalu
Awali ya yote, niwapongeze wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kufuata ushauri wangu niliowausia wiki iliyopita kupitia safu hii. Ni kuhusu uchaguzi wa viongozi wa vikao vyenu, kwa maana ya spika na naibu wake. Mmefanya uchaguzi sahihi, niliyowaandikia mmeyafanya kwa vitendo. Hongereni sana.
Awali ya yote, niwapongeze wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kufuata ushauri wangu niliowausia wiki iliyopita kupitia safu hii. Ni kuhusu uchaguzi wa viongozi wa vikao vyenu, kwa maana ya spika na naibu wake. Mmefanya uchaguzi sahihi, niliyowaandikia mmeyafanya kwa vitendo. Hongereni sana.
Sina shaka na uwezo wa Spika, Job Yustino Ndugai wala sipati tabu na
weledi wa Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson Mwansasu. Hawa ni wazalendo,
hivyo vikao vya bunge vitaendeshwa kwa haki.
Dhumuni la makala haya kwa leo nataka niwekane sawa kidogo na Waziri
Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa. Kwanza nakupongeza kwa kuteuliwa kwako
na Rais John Pombe Joseph Magufuli, pia na kuthibitishwa na wabunge kwa
asilimia zaidi ya 70. Hii inaonesha ni kwa namna gani wana imani na
wewe, wanakujua kwa undani juu ya weledi wako kikazi.
Binafsi, siwezi kuzungumza chochote juu ya ufanisi wako wa kazi,
sijawahi kukufuatilia kwa ukaribu kiasi cha kuweza kutoa maoni ya ama u
mahiri katika kazi au kinyume chake. Siwezi. Sitaki kuwa mnafiki.
Hata hivyo, wewe ulishangazwa na uteuzi huo maana nakumbuka moja kati ya
kauli uliyotoa muda mfupi baada ya jina lako kusomwa bungeni na spika
ni kuwa, ulilia maana hukutarajia, huo ni ukweli. Miongoni mwa majina ya
wanasiasa waliokuwa wakipigiwa chapuo, jina lako halikuwahi kutajwa
mara kwa mara kama wengine.
Achana na hayo, hoja yangu hapa nataka niijenge juu ya utayari wako
kuhusu kuendana na kasi ya bosi wako, Rais Magufuli. Nimesikiliza kwa
umakini sana hotuba yako ya kuahirisha kikao cha kwanza cha Bunge la 11.
Uliwaahidi wabunge kuwa utashirikiana nao katika kutekeleza majukumu
yako na kwa Watazania. Ulisema utafanya kazi kwa bidii na kwa weledi
mkubwa kama ulivyoelekezwa na Rais Magufuli.
Hapo ndipo nilipatwa na swali tata kuwa kumbe ulielekezwa nini cha
kufanya na Rais Magufuli na si kwamba wewe mwenyewe unajua nini
unatakiwa kukifanya kwa Watanzania? Swali ni kwamba, ina maana kila
utakachokuwa unakifanya kitatokana na maelekezo ya rais? Sitaki kuliweka
sana akilini jambo hilo.
Kasi ya Rais Magufuli ni ya juu mno. Hotuba aliyoitoa wakati akilifungua bunge hilo iliashiria kabisa jinsi alivyopania kuleta mabadiliko na mapinduzi ya kweli kwa taifa letu. Ilionesha ni kwa namna gani mambo yatakavyoendeshwa kwa mchakamchaka mkubwa.
Kasi ya Rais Magufuli ni ya juu mno. Hotuba aliyoitoa wakati akilifungua bunge hilo iliashiria kabisa jinsi alivyopania kuleta mabadiliko na mapinduzi ya kweli kwa taifa letu. Ilionesha ni kwa namna gani mambo yatakavyoendeshwa kwa mchakamchaka mkubwa.
Kwa nafasi uliyopewa, wewe ndiye mtendaji mkuu wa shughuli za serikali.
Wewe ndiye mhimili mkuu. Sasa nabaki najiuliza, kwa hali inavyoonekana
kasi hiyo ya Magufuli utaendana nayo bila kupunguza wala kulegea?
Siulizi swali hili kwa maana ya kutokuwa na imani na wewe la hasha! Ila
kasi ya Magufuli inahitaji utashi wa hali ya juu na zaidi ya utendaji wa
kawaida. Mbio za utendaji kazi wake ni za kasi ya juu mno na ukiwa
waziri mkuu unapaswa kuendana nayo sambamba. Je, unao utayari huo? Gari
lako katika kasi hiyo ya utendaji kazi wa Magufuli lina mafuta ya
kutosha?
Wapo waliosema, unatosha na unafaa sana kushika nafasi hiyo kutokana na
utendaji kazi wako. Hawa ni wale uliofanya nao kazi kwa ukaribu katika
nyanja mbalimbali za utumishi kabla ya kutunukiwa nafasi hiyo ya juu.
Ushauri wangu kwako hakikisha gari lako lina mafuta ya kutosha kuendana
na kasi ya Rais Magufuli ili lisije likazimikia njiani kwa kushindwa
kuhimili umbali wa safari na mwendokasi wa bosi wako
Tumia kila aina ya weledi ulionao katika utumishi, fanya kazi kwa
ukaribu na wananachi, usimuonee haya waziri atakayeonekana anavurunda
katika utekelezaji wa majukumu yake, usije ukaangukiwa na jumba bovu
maana Magufuli sitarajii kuona haya kukusema ukienda kinyume na
matarajio yake na hilo halitakufurahisha.
Ni hayo tu kwa leo, vinginevyo nakutakia utekelezaji mwema wa majukumu
yako kwa nafasi hiyo nyeti katika utumishi wa umma. Mungu akutangulie.
Nawasilisha.

Note: Only a member of this blog may post a comment.