Rais John Magufuli.
Na Elvan Stambuli
KUTOKANA na hotuba kali na yenye matumaini aliyoitoa Rais John Magufuli mwishoni mwa wiki wakati anafungua Bunge la 11, baadhi ya viongozi wa dini wameshauri kiongozi huyo wa nchi aongezewe ulinzi.
KUTOKANA na hotuba kali na yenye matumaini aliyoitoa Rais John Magufuli mwishoni mwa wiki wakati anafungua Bunge la 11, baadhi ya viongozi wa dini wameshauri kiongozi huyo wa nchi aongezewe ulinzi.
Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati
tofauti, viongozi hao walisema Magufuli ni mchapakazi na kauli yake ya
kupambana na mafisadi ni nzuri lakini inapaswa iende sambamba na ulinzi
wa kutosha.
Katibu Mkuu wa Mashehe na Wanazuoni nchini, Shehe Hamisi Mataka alipohojiwa na gazeti hili alisema:
“Rais Magufuli ni tunu ya taifa, Waziri
Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa ni mchapakazi, inafaa walindwe kuliko
kawaida kwa sababu kazi wanayoifanya ni ya taifa kwa faida ya taifa.
“Wote hawa nawafahamu ni wachapakazi na wana nguvu ya kutumikia taifa kwani wote hufuatilia kazi na siyo watu wa kukaa ofisini.”
Alisema anamuombea Rais Magufuli na
waziri mkuu wake afya njema ili waweze kutumikia taifa kama walivyoahidi
na ana imani kuwa Watanzania watagundua baada ya siku si nyingi kwamba
hawakufanya makosa kumchagua kuongoza nchi.
Akimzungumzia Waziri Mkuu, Majaliwa, Shehe huyo alisema ni mtu anayeweza kuendana na kasi ya Magufuli.

Note: Only a member of this blog may post a comment.