Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Chama cha Madereva Bodaboda Wilaya ya Temeke, Said Kagomba, amesema kuwa taarifa za uvumi ulioenea mtaani si za kweli na hakuna taarifa yoyote kutoka kwao ya kuitisha maandamano kwa madereva kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu yaliyotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Amesema kuwa, madereva bodaboda hawana mamlaka ya kufanya maandamano kwani vyama vya madereva havijihusishi na masuala ya siasa, hivyo taarifa zilizopo mtaani si za kweli na zinapaswa kupuuzwa mara moja.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Madereva Wilaya ya Ilala, Soud Komba, amewatahadharisha madereva bodaboda kutojiingiza kwenye masuala ya kisiasa kwa kufanya maamdamano kwa madai yakuwa kufanya hivyo ni kusababisha uvunjifu wa amani hapa nchini na kuwataka kuwapuuza wanasiasa wanaoweza kuwashawishi kwa matakwa yao binafsi.
(NA DENIS MTIMA/GPL)

Note: Only a member of this blog may post a comment.