Wednesday, November 4, 2015

Anonymous

VIDEO&PICHAZ: Tazama Mechi za UEFA CHAMPIONS League Zilivyokua Jana Usiku!


Mechi za Ligi ya Mabingwa Ulaya zimeendelea tena usiku wa November 3 kwa mechi kadhaa kupigwa katika viwanja nane kwa michezo ya Kundi A, B, C na D kupigwa. Hizo ni mechi za marudiano za timu zilizopo katika makundi husika, Klabu ya Manchester City ya Uingereza ililazimika kusafiri hadi Hispania kuifuata Sevilla.

Manchester City ya Uingereza imefanikiwa kuvuna point tatu katika mchezo huo pamoja na jumla ya idadi ya magoli matatu, Kwa maana hiyo Man City iliyopo Kundi D lenye timu za Juventus, Sevilla na Borussia Moenchengladbach imetimiza jumla ya point tisa na kushika nafasi ya kwanza.

Mchezo umemalizika kwa Man City kuibuka na ushindi wa goli 3-1, magoli ya Man City yalifungwa na Raheem Sterling dakika ya nane, Fernandinho dakika ya 11 na Wilfried Bony dakika ya 36 baada ya Sevilla kufunga goli moja pekee dakika ya 25 kupitia kwa Benoit Tremoulinas.
Video ya magoli ya Sevilla Vs Man City  
Real Madrid Vs PSG
Manchester United Vs CSKA Moscow

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.