Bernard Paul ‘Ben Paul’.
UKIACHANA na vyombo vya muziki, kingine kinachombeba
msanii ni ubora wa sauti yake na hata akiimba ‘live’ basi ladha yake
hupenya zaidi kwenye masikio ya wasikilizaji. Tanzania tumejaaliwa kuwa
na wasanii wazuri wenye sauti zenye mvuto lakini wengi wao hupotezea
sanaa hiyo na kuamua kujikita katika maisha mengine ya kujitafutia
kipato.
Ali Kiba.
Sabau kubwa inayowaondoa katika muziki ni kukatishwa tamaa na
mapromota wachache wanaojali maslahi yao binafsi na kumuacha msanii
akipata shida.Ukiangalia kwa upande wa ‘mamtoni’, wasanii wamekuwa
wakichukulia muziki kama kazi na ndiyo wanaingiza kiasi kikubwa sana cha
fedha.
Mfano mzuri ni P Diddy, leo hii anamiliki helikopta, boti na vitu
vingine vingi kutokana na muziki.Wale wenye sauti tamu kama Ne-yo, Chris
Brown, Trey Songz na wengineo kibao wamekuwa wakisaidia kutusahaulisha
maisha ya shida kupitia muziki wanaoufanya.
Yote tisa, kumi msanii bila kufanya kolabo (ushirikiano katika
nyimbo) na wenzako mara nyingi mashabiki wako wanakuwa wanashindwa
‘kujaji’ uwezo wako.Hapa nakuletea wasanii wa Tanzania ambao ukiwapa
kolabo hasa kwenye kuimba kiitikio hakika hutembea mulemule na wanaweza
kumtoa chipukizi au msanii mgeni kwenye tasni hiyo;
Anasifika kwa sauti matata ambayo wengi
hupenda kuisikia akiimba ‘live’ kwani hiyo ‘vocal’ yake ni noumaaaa!
Angalia kazi anazoshirikishwa na namna anavyozitendea haki.Amefanya
kolabo nyingi sana na zote amekimbiza na nyingine kuwafunika kabisa
wahusika wakuu wa nyimbo.Baadhi ya ngoma alizoshirikishwa na kufanya
vizuri ni Nai Nai aliompa sapoti Ommy Dimpoz na kumtambulisha kisanaa,
Msambinungwa ya Tundaman hapo bado haijatajwa Hands Across the World
aliofanya na wakali kibao kutoka Afrika na mkali wa R&B, Robert
Kelly wa Marekani. Asilimia kubwa ya ngoma anazoshirikishwa huwa
zina-hit.
Elias Barnabas kijana ana umbo dogo lakini kazi yake ni kubwa sana. Ni
zao la Tanzania House of Talent (THT), amekuwa akitoa sapoti kubwa sana
kwa wenzake.Pia amefanya kazi nyingi sana na ana uwezo wa kufunika
vilivyo kwenye kazi anazoshirikishwa. Amefanya kolabo na Izzo Biznes
Ngoma ya Love Me akiwa na Shaa,Nivute Kwako ya Dayna, Natumaini
aliyopewa shavu na
Beka, Zamani remix ya Q Chillah na nyingine kibao. Mara nyingi
hachagui kufanya kazi na mtu cha msingi anazingatia kama una kipaji
ndipo anakupa nafasi ya kukubusti kwa kutumia sauti yake.
DULLY SYKES
Jina lake kamili ni Abdul Abby Sykes, ana umri wa miaka 34, ukitaja kati ya listi ya wasanii wa Bongo Fleva ambao wamedumu zaidi kwenye sanaa hiyo basi hutaacha kutaja jina lake. Hii yote ni kutokana na kazi yake kukubalika na watu wa aina tofauti kuanzia watoto na watu wazima. Amejitahidi sana kuwaibua wasanii wengi ambao wamepitia kwenye studio yake ya Dhahabu Records lakini pia jamaa sio mchoyo wa kolabo, ukimpa nafasi akuimbie kiitikio basi ni lazima akamue na ngoma inafanya vizuri ikiwa tofauti basi ni mapenzi ya Mungu. Ameshiriki katika Ngoma ya Action ya C Pwaa akiwa na Ms Trinit na Ngwair, Mdananda wa Shetta, Manenomaneno wa Queen Darleen na nyingine kibao lakini sasa tazama nyimbo zake zinavyochana spika mitaani hatari sana!

BEN POL
Wazazi wamempa jina la Bernard Paul
Mnyelange, sasa hivi anatesa na Wimbo wa Sophia, naye ameingia kwenye
listi ya wasanii ambao pengine wanafanya vizuri kila wanaposhirikishwa
na wenzake. Alifanikiwa kutwaa Tuzo mbili za Kili kama Mwimbaji Bora wa
R&B 2011-2012 kupitia ngoma zake za Nikikupata na My Number One Fun.
Baadhi ya Ngoma alizoshirikishwa ni Mama Yeyo ya G Nako, Sitaki Kazi ya
Nikki wa Pili, Sikati Tamaa ya Darasa na
zote amekamua kwenye kolasi na inaonyesha jamaa yupo vizuri kikazi.
zote amekamua kwenye kolasi na inaonyesha jamaa yupo vizuri kikazi.
G NAKO
Jina lake la kazini anaitwa George Sixtus
Mdemu a.k.a G Nako. Nani asiyemfahamu msanii huyu kwa sasa? Bonge moja
la msanii ambaye kolabo yoyote anakaa, jamaa anatokea Kundi la Weusi na
asilimia kubwa amekuwa akihusika kuimba kolasi za ngoma za kundi hilo.
Amefanya nyimbo nyingi na wasanii wenzake na akatusua kama Mfalme ya
Mwana FA, XO ya Joh Makini, Bum Kubam aliyoshirikishwa na Nikki wa Pili,
Tumewaka aliyompa sapoti Godzilla na nyingine nyingi

Note: Only a member of this blog may post a comment.