Gladness Mallya
STAA wa filamu za Kibongo, Shamsa Ford amewataka
wasanii wenzake waliotofautiana wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu
uliofanyika Oktoba 25, mwaka huu kumaliza bifu kwani zoezi hilo
limemalizika na maisha lazima yaendelee.
“Jamani wasanii wenzangu mliotofautiana na kuwekeana bifu kipindi cha uchaguzi, nawasihi mmalize ili tufanye kazi kwa bidii kwani wakati wote wa kampeni tasnia ya filamu ilikuwa imelala,mimi nimeshaanza kwa kasi ya ajabu na hivi karibuni filamu yangu mpya itakuwa mtaani,” alisema Shamsa.

Note: Only a member of this blog may post a comment.