Wednesday, November 4, 2015

Anonymous

Hali ya Mzee MKAPA! Spika wa Bunge TZ?! TB Joshua TZ? Marais Watakaomshuhudia DK. Magufuli? (Audio)

Good Morning mtu wangu, Uchambuzi wa magazeti redioni @CloudsFM umekupita? Kazi yangu siku zote ni kuhakikisha zile zote kubwa za siku zinakufikia, hizi ni baadhi ya zilizogushwa kwenye Uchambuzi redioni. 

Nabii TB Joshua na Marais nane kushuhudia sherehe za kuapishwa Dk. John Magufuli, orodha ya Wabunge viti maalum hadharani, TB Joshua ateta na Lowassa na Magufuli, Samuel Sitta kuwania Uspika wa Bunge la 11, Mkapa taharuki, taarifa za ugonjwa wa kifo juu yake zasambaa Dar, Ikulu yatoa ufafanuzi na Makamishna wa ZEC waendelea kubanwa. 

Ikulu imesema Rais Mstaafu Mzee Benjamin Mkapa ni mzima mwenye afya na taarifa zote zinazosambaa mitandaoni kuhusu kuugua kwa Rais huyo mstaafu sio za kweli, ni uzushi. 

Marais nane wa Africa ni miongoni ya watu watakaoshuhudia sherehe za kuapishwa Rais wa awamu ya tano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli siku ya tarehe 5 November 2015 kwenye uwanja vya Uhuru jijini Dar es salaam, miongoni ya Marais hao ni, Paul Kagame wa Rwanda, Robert Mugabe wa Zimbabwe, Uhuru Kenyatta wa Kenya na Yoweri Museveni wa Uganda. 

Wakati vikao vya Bunge la 11 vikitegemea kuanza wiki ijayo mjini Dodoma, Samuel Sitta, Anna Makinda na Zungu kuchuana tena kwenye nafasi ya Uspika wa Bunge hilo lijalo… Wakazi wa jiji la Arusha wamemtaka Rais Mteule Dk. John Magufuli kuhakikisha anasimamia uwajibikaji kwa kila Mtanzania kwa kupiga vita baa na vijiwe vya kahawa kufunguliwa wakati wa kazi. 

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Dar es salaam, Paul Makonda ameunda Kamati ya Maadili ya Mahakama ya Mwanzo katika Wilaya hiyo ambayo jukumu lake ni kuwabaini na kuwawajibisha Mahakimu wote ambao watakwenda kinyume na maadili ya kazi zao.

Unaweza pia kusikiliza uchambuzi wote wa magazeti kwenye #PowerBreakfast hapa chini kwenye hii sauti.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.