Wema Sepetu akiwa ndani ya gari lake jipya.
STORI: MUSA MATEJA NA IMELDA MTEMA
WEMA Isaac Sepetu ‘Madam’ ameangusha
bethidei baab’kubwa ambayo imesheheni kufuru ya aina yake na ‘kumtusi’
hadharani mpenzi wake wa zamani, Nasibu Abdul ‘Diamond’ kwa kumsema kuwa
ni mtu wa kununua magari ya bei rahisi hivyo hawezi kuifikia hadhi
yake, Risasi Mchanganyiko lina mchapo kamili.
Staa wa Bongo Fleva Nasibu Abdul ‘Diamond’.
ILISOGEZWA MBELE MAKUSUDI
Sherehe hiyo ambayo ilikuwa ifanyike
Septemba 28, mwaka huu ambayo ndiyo siku ya kuzaliwa Madam, ilisogezwa
mbele makusudi kutokana na ubize aliokuwa nao wa kukifanyia kampeni
Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kuamua kuifanya Jumapili iliyopita (Novemba
1) baada ya kumalizika kwa shughuli hiyo iliyoisha kwa ushindi wa
mgombea urais wa CCM Dk John Magufuli.
Sherehe hiyo iliyosheheni mastaa kibao
Bongo, ilifanyika katika ukumbi wa Wema Sepetu uliopo ndani ya jengo la
Millenium Towers, Kijitonyama jijini Dar ambapo mwanadada
huyo alizua gumzo la aina yake baada ya kujizawadia gari aina ya Range Rover lenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 200.
MASTAA WAANGUSHA BURUDANI
Mbali na kusheheni vyakula vyenye hadhi
ya juu, kwenye sherehe hiyo walikuwapo mastaa mbalimbali wa Bongo Fleva
kama Barnaba Elias, Ali Kiba, Vanessa Mdee na Sam Machozi ambao
walitumbuiza nyimbo mbalimbali kusherehesha pati hiyo.
KEKI ZA KUMWAGA
Kuonesha kwamba amedhamiria kuwakomesha,
keki kubwa kwenye sherehe hiyo zilikuwa tano sambamba na ndogondogo
zaidi ya 20 ambazo zilipambwa katika meza aliyokaa Wema na kuvutia.
MAVAZI MEUPE YATAWALA
MAVAZI MEUPE YATAWALA
Waalikwa kwenye sherehe hiyo walionekana
kufunikana kwa kuvaa mavazi meupe yenye mvuto wa tofauti hivyo kuufanya
ukumbi mzima kuonekana mweupe.
ZAWADI SASA
Ulipofika wakati wa zawadi, mastaa na
waalikwa mbalimbali walishindana kumtunza mrembo huyo asiyechuja Bongo,
vitu mbaimbali vya thamani, zikiwemo fedha taslimu ambapo ‘wekundu wa
Msimbazi’ walionekana kutapakaa katika eneo maalum la kupokelea zawadi
alilokaa Madam.
AMTUSI DIAMOND
AMTUSI DIAMOND
Mara baada ya kukamilika kwa zoezi la
zawadi ndani ya ukumbi, ndipo Wema alipowatoa nje waalikwa na
kuwaonyesha gari lake jipya aina ya Range Rover ambalo linasadikika kuwa
litakuwa la kwanza kumilikiwa na msanii wa kitanzania kutokana na
thamani yake.
“This is my new brand car, yaani ni mpya ya mwaka 2015, hakuna kenge yeyote anayeweza kufuata nyendo zangu na yule ambaye alikuwa akijigamba eti alinipa zawadi ya gari la elfu 30, nini na nini na hili aseme sasa maana mimi si wa kuhongwa kila kitu,” alisema mrembo huyo, kauli iliyoonyesha wazi kumlenga Diamond, ambaye aliwahi kumzawadia Wema gari lenye thamani ya shilingi milioni 30 miaka michache iliyopita.
“This is my new brand car, yaani ni mpya ya mwaka 2015, hakuna kenge yeyote anayeweza kufuata nyendo zangu na yule ambaye alikuwa akijigamba eti alinipa zawadi ya gari la elfu 30, nini na nini na hili aseme sasa maana mimi si wa kuhongwa kila kitu,” alisema mrembo huyo, kauli iliyoonyesha wazi kumlenga Diamond, ambaye aliwahi kumzawadia Wema gari lenye thamani ya shilingi milioni 30 miaka michache iliyopita.
Gari aina ya Range Rover alilonunua Wema.
AANIKA GHARAMA ZA GARI
“Naomba niwaambie kuwa hadi naifikisha
hapa, hii gari nimetumia zaidi ya dola elfu 90 za Kimarekani, sijahongwa
na mtu, ni pesa yangu kwa nguvu zangu mwenyewe, nawaomba mpande ndani
mshuhudie ziro kilometa (halijatumika).
NI GARI LA NDOTO ZAKE
NI GARI LA NDOTO ZAKE
kwa hatua hii maana ilikuwa ni gari ya
ndoto zangu, na leo namshukuru Mungu yangu mwenyewe, hakuna anayeweza
kugusa hapa inaitwa piga kimya, ni mpya ambayo natarajia kuanza kuchana
karatasi zake kuanzia kesho,” alisema Madam.
Baadhi ya waalikwa ambao walishuhudia
shughuli hiyo na mama mzazi wa mrembo huyo Miriam Sepetu, kusema
ameandaa hafla ya kistaa, ambayo inaendana na hadhi yake.
“Daah kuanzia ukumbi ulivyopambwa, gari
alilojinunulia, vyakula na vinywaji ni balaa. Hakuna mfano sijaona pati
ambayo wahudhuriaji.
WALIOHUDHURIA
WALIOHUDHURIA
Sherehe hiyo iliyohudhuriwa na wadau
mbalimbali wa burudani, ilipambwa na mastaa wengi akiwemo mtangazaji
Hamis Mandi ‘B 12’, Idriss Sultan, Martin Kadinda, Elizabeth Michael
‘Lulu’, Halima Yahya ‘Davina’ na Steven Mengere ‘Steve Nyerere’.

Note: Only a member of this blog may post a comment.