WATU watano waliokuwa wakichimba madini katika mgodi wa Nyangarata
uliopo Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga wamepatikana wakiwa hai baada
ya kufukiwa na vifusi kwenye mashimo ya mgodi huo kwa siku 41.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Ofisa Habari wa Wizara ya Nishati na Madini, Badra Masoud amesema kuwa wachimbaji hao wanaodaiwa kuwa sita, walifukiwa na vifusi mnamo Oktoba 5, mwaka huu na kuendelea kuishi kwenye mashimo hayo huku wakila magome ya miti, vyura na udongo baada ya kushiwa chakula walichokuwa nancho, hadi jana Novemba 5, walipookolewa umbali wa kilomita 10 ndani ardhini na watano kati yao kukutwa hai huku mwenzao mmoja akidaiwa kufariki dunia.
Baada ya kupatikana wakiwa hai, manusra hao walikimbizwa kwenye Hospitali ya Wilaya ya Kahama ambako wanaendelea kupata matibabu.
Badra amewataja waliopatikana hai kuwa ni; Joseph Bulule, Chacha Wambura, Unyiwa Aindo, Msafiri Gerald na Muhangwa Amos. Wakati aliyefariki akimtaja kwa jina la Mussa Supana.

Note: Only a member of this blog may post a comment.