POLE! Staa mwenye mvuto ndani ya Bongo Muvi, Kajala Masanja hivi
karibuni alipata pigo zito baada ya kufiwa na bibi yake (mzaa mama)
aliyekuwa akiuugua kwa muda mrefu huko mkoani Songea.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda akiwa msibani, Kajala alisema
amempoteza mtu muhimu katika maisha yake kwani bibi yake huyo alikuwa
akimpenda, kumlea na kumshauri mambo muhimu kwenye maisha.
“Siwezi kueleza ni jinsi gani nilikuwa nikimpenda bibi yangu, alikuwa ni msaada mkubwa sana kwangu.
Kila nilipotatizika na jambo lolote sikusita kumfuata na kumshirikisha, kiukweli ni pigo kubwa sana kwangu,” alisema Kajala.
Staa mwenye mvuto ndani ya Bongo Muvi, Kajala Masanja.
Kajala
alifunguka kuwa alipopata taarifa za msiba wa bibi yake alihisi
kuchangayikiwa na maumivu yaliyosababisha mapigo ya moyo kupanda
(presha).“Siwezi kueleza ni jinsi gani nilikuwa nikimpenda bibi yangu, alikuwa ni msaada mkubwa sana kwangu.
Kila nilipotatizika na jambo lolote sikusita kumfuata na kumshirikisha, kiukweli ni pigo kubwa sana kwangu,” alisema Kajala.
Note: Only a member of this blog may post a comment.