Wednesday, August 12, 2015

Anonymous

WAMENASWA! Huu Ndio UCHAFU wa Mabamedi Jijini Dar

http://api.ning.com/files/rYXJV*jyRSlygLmryaKBo50Qnd3di7PFjJ16UJk9hBdftoKgkAV-UOqYpwbzynwOgCk6eqFkYHLLnKqCycnO-oAd8O4aXaht/OFM.gif
Chande Abdallah na Deogratius Mongela

WAMENASWA! Kitengo maalum cha Oparesheni Fichua Moavu (OFM) cha Global Publishers mwishoni mwa wiki kiliwanasa wahudumu wa baa wakiuzwa kwa wanywaji wanaohitaji huduma ya ngono katika mtego uliofanywa katika baa moja iliyopo Ubungo External, Ilala jijini Dar es Salaam. 
OFM yanasa mabamedi wakijiuza
Awali, mtoa habari wetu alikiambia kitengo hicho kuwa wako wahudumu wengi wa mabaa mbalimbali jijini Dar es Salaam wanaojiuza na kwamba wanafanya hivyo kwa kuwa wanapata baraka kutoka kwa viongozi wao (mameneja) ambao huwaruhusu kuondoka wakati wowote wakiwa kazini kwa makubaliano ya malipo ya shilingi elfu mbili (2000).

“Ukishalipa hiyo hela unaondoka naye na huko sasa ndiyo mnapoelewana wenyewe kama mtalipana kiasi gani kabla ya kufanya mapenzi, kifupi wengi wa wahudumu wa kwenye baa ni kama machangudoa, ile kazi ni utambulisho tu,” kilisema chanzo hicho na kuzitaja baa kadhaa jijini Dar zenye mtindo huo hasa za maeneo ya Ubungo, Tandale, Buguruni, Tandika na Mbagala Rangi Tatu.

Baada ya kuzinyaka taarifa hizo, OFM iliingia kazini na kuanza na baa moja maeneo ya Ubungo External, lakini cha kushangaza, ilikutana na wahudumu wa kiume tu, ambao walisema wenzao wa kike walikuwa wameondoka na wateja.

Katika baa ya jirani yake, OFM ilifika na kuagiza vinywaji kama kawaida, kabla ya kuingia mzigoni kwa kumtongoza mhudumu mmoja wa kike, ikitaka kuondoka naye muda uleule.
OFM: Mambo vipi?

BAAMEDI: Poa.

OFM: Njoo ukae hapa kuna jambo nataka kukueleza.

BAAMEDI: Mh! Siwezi kukaa, (huku akisogea na kumpa sikio Kamanda) haya niambie.

OFM: Nimevutiwa sana na wewe, naweza kukupata saa hivi?

BAAMEDI: Mh! Hapana, labda baadaye kwa sababu sasa hivi tuna wateja wengi, tupo bize sana.

OFM: Nitakupata muda gani?

BAAMEDI: Saa 4 hivi nitakuwa poa.

(alisema baamedi huyo huku akiondoka baada ya kuitwa meza nyingine).

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.