Tuzo za All Afrika Music Awards 2015 (AFRIMA) zimetolewa usiku wa
Jumapili November 15 jijini Lagos, Nigeria ambapo Tanzania imetoa
washindi wawili.
Diamond Platnumz aliyekuwa akiwania tuzo hizo ameibuka mshindi wa
vipengele 3 kikiwemo kipengele muhimu cha Msanii Bora Wa Mwaka
(Artist Of The Year) ambayo ilikuwa ikiwaniwa na Alikiba, Davido, Jose
Chameleone, Wizkid, Yemi Alade, Sarkodie na Flavour.
Vipengele vingine alivyoshinda Diamond ni Msanii Bora wa Kiume
Afrika Mashariki (Best Male Artist in Eastern Africa) pamoja na Wimbo
Bora Afrika (Nasema Nawe).
“Jus wanted to let you know that we have won the first one BEST EAST
AFRICAN ARTIST OF THE YEAR! this isnfor you my fans… thanks for the
Votes!!! thanks alot @the_speshoz for this Suit and many thanks to my
brother @jm_international_collection for the scarf and Tie!
#AfrimaAwards” alindika Diamond Instagram.
Vanessa Mdee ameshinda kipengele cha ‘Best African Pop’ kupitia wimbo wake ‘Hawajui’.
GLORY TO GOD IN THE HIGHEST! #BestAfricanPop #Hawajui thankyou @nahreel @barnabaclassic and… https://t.co/0HquLG0sb8
— VeeMoneyNeverEver (@VanessaMdee) November 15, 2015
Msanii mwingine wa Tanzania aliyekuwa akiwania tuzo hizo ni Linah,
ambaye alikuwa akishindania kipengele cha Msanii Bora Wa Kike Afrika
Mashariki hakubahatika kushinda kipengele hicho.
Note: Only a member of this blog may post a comment.