Asubuhi yako inaendaje mdau wangu? Inawezekana uchambuzi wa magazeti @CloudsFM umekupita, kama hukuzipata zote zilizosikika kwenye kuperuzi na kudadis nilizozirekodi zote ziko hapa unaweza kuzipitia kufidia zilizokupita.
Kamati kuu ya CCM imepitisha majina matatu kati ya wagombea 21 waliyojitokeza kuwaninia nafasi ya Uspika wa Bunge la 11 la Tanzania majina hayo ni, Job Ndugai, Dk. Tulia Ackson Mwansasu na Abdallah Ali Mwinyi, wengine waliyokuwa wanawania nafasi hiyo ni pamoja na Samuel Sitta, Dk. Kalokola na Dk. Didas Masaburi ambaye alitangaza kujitoa katika dakika za mwisho.
Wakati kitendawili cha kwanza kinatarajiwa kuteguliwa tarehe 19 November 2015 mjini Dodoma, pale Bunge la 11 litakaporidhia uteuzi wa Waziri Mkuu anayesubiriwa kwa hamu, mtihani mwingine kwa Rais Dk. John Magufuli unabaki kwenye uteuzi wa Baraza la Mawaziri.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza, jana lililazimka kupiga mabomu ya machozi katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando (BMC), ili kuwatawanya wafuasi wa CHADEMA waliokuwa wameupokea mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Geita, Alphonce Mawazo aliyeuawa kwa kukatwa mapanga.
Soko la samaki Feri
kurekibisha majiko yake ya samaki ambayo kwa muda mrefu moshi wake
umekuwa ukisababisha kero kubwa kwenye ofisi mbalimbali za umma ikiwemo Ikulu... Matukio ya ujambazi unaofanana na ule wa Panya Road umeibuka tena jijini Dar es salaam ambapo majambazi hao wanavamia maduka mbalimbali mtaani wakiwa na silaha za moto.
Aliyekuwa mgombea wa nafasi ya Urais kupitia ticket ya CHADEMA na UKAWA, Edward Lowassa
amesema amepoteza pambano na sio vita hivyo ataendelea kushiriki
kikamilifu kwenye shughuli za kisiasa na kubainisha kuwa ataendeleza
mapambano ya mabadiliko kwa kuwekeza nguvu kubwa kwenye mchakato wa
kusaka Katiba mpya.
Tunaomba radhi kutokana na tatizo la sauti.
Note: Only a member of this blog may post a comment.