Tanzania ni moja kati ya nchi ambazo
zimeathirika sana na ishu ya ujangili wa wanyamapori… vita imeanzia
Afrika na duniani kwa ujumla ambapo jitihada mbalimbali zimefanywa
kuhakikisha biashara inayohusisha wanyama kama tembo inapigwa marufuku.
Taarifa imeripotiwa na Kituo cha ITV
inahusu mradi wa kimataifa wa kuboresha mtandao wa maeneo ya hifadhi na
ambapo tembo wanafungwa vifaa maalum vya kisasa kwa ajili ya
kuwafatilia na kuwapa ulinzi.
Kazi tayari imeanza, zoezi la tembo
kufunga vifaa hivyo limeanzia katika hifadhi ya taifa ya Ruaha pamoja na
pori la akiba la Rungwa.
Story iko kwenye hii sauti pia kutoka kwenye habari ya Kituo cha ITV.

Note: Only a member of this blog may post a comment.